• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DODOMA NA DHAMIRA YA DHATI YA KILIMO CHA TUFAA (APPLE)

Imetumwa : May 12th, 2025

Na. Sizah Kangalawe 

Habari – DODOMA RS

Ni matamanio ya viongozi kuona uchumi wa Wananchi wanaowaongoza unaongezeka kwa kasi na unakua wa kuridhisha hususani katika pato la Mwananchi mmoja mmoja na eneo husika.

Uongozi wa Mkoa wa Dodoma Ukiongozwa na Mhe. Rosemary Senyamule, unayo matarajio, matumaini, nia na dhamira ya dhati  ya kukuza pato la wananchi wa Mkoa huu pamoja na pato la Mkoa kwa ujumla wake.

Ili kuyafanikisha hayo Mkoa umeanza jitihada mbalimbali za kuhakikisha ndoto na nia zao za dhati zinatimia ikiwa ni pamoja na kufanya tafiti mbalimbali za kitaalamu juu ya nini kinaweza kuwakwamua wananchi wake kutoka katika wimbi la umaskini na kuwa katika uchumi wa kati hadi uchumi wa juu.

Mkoa wa Dodoma umedhamiria kuanzisha kilimo biashara cha zao la  tunda maarufu la tufaa (apple) kwani kutokana na utafiti uliofanyika, zao hilo linaweza kustawi katika ardhi ya Dodoma na likaleta matokeo ya kuridhisha.

Ili kufanikisha kilimo hicho Mkoa umechukua jitihada mbalimbali ikiwemo kusafiri umbali wa zaidi ya KM 310 kutoka Dodoma - Ifunda, Mkoani Iringa katika Shamba la Tamu Tamu Tanzania, mahali ambapo uzalishaji wa Miche ya tufaa pamoja na bidhaa mbalimbali zinazotokana na tunda hilo unafanyika.

Lengo la ziara hiyo ni kujifunza kwa vitendo namna kilimo hicho kinavyofanyika kitaalamu pamoja na kujifunza namna sahihi ya kuendesha kilimo hicho, ikiwa ni pamoja na kujua aina zinazostahimili hali ya hewa ya Dodoma, mbolea na viuatilifu vinavyostahili n.k.

Akizungumza wakati wa Ziara hiyo, Mhe. Senyamule amesema ‘’ Tumekuja hapa na tumejifunza, tumehamasika na tumepata ari kuwa kumbe mawazo yetu, yanaweza yakawa ni mapinduzi ya kiuchumi kwa wananchi wa Mkoa wa Dodoma hasa uchumi wa Mwananchi mmoja mmoja.

‘’Sisi leo tumekuwa ni watu wenye furaha sana kuwa tunaanza kuona ndoto tunayoifikiria kwa ajili ya wananchi wa Dodoma, tunayoiona Dodoma ya Miaka 5 ijayo, tunaona watu wenye furaha, Uchumi lakini sisi kuzalisha tu bali tuanzishe na viwanda vya kuliongezea thamani zao hili, soko bado lipo nchini na nchi za wenzetu pia’’, amesema Senyamule.

Aidha Mhe. Senyamule ameweka bayana maazimio ya ziara hiyo kuwa ni pamoja na zao hilo kuwa miongoni mwa mazao ya Mkoa, kuanzisha kilimo hicho kabal ya 2025 kumalizika,  kila Halmashauri kuanzisha shamba darasa kuanzia hekari 1 yenye miundombinu ya umwagiliaji pamoja na kuwapeleka maafisa ugani wa wilaya kupatiwa mafunzo juu ya zao hilo.

Akizungumza kwa niaba ya Wakuu wa Wilaya, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Alhaji Jabir Shekimweri amekiri unafuu wa uzalishaji wa zao hilo ukilinganisha na mazao mengine ya kibiashara yanayolimwa Mkoani Dodoma.

‘’Zao hili la Tufaa (Apple) gharama zake za uzalishaji ziko chini ukilinganisha na shamba la zabibu, kwaiyo sisi kama Wilaya  tumeichukulia ziara hii kwa uzito unaostahili   na sisi kama Jiji tayari tunayo maeneo tuliyoyatenga ya kuanzia uzalishaji wa zao hili ambalo tunatarajia ndio litakalo kuwa mbadala au ziada ya Zabibu’’, Mhe. Shekimweri

Ziara hiyo ya siku moja iliwajumuisha Viongozi wa Mkoa (Mkuu wa Mkoa  na Katibu Tawala Mkoa), Wakuu wa Wilaya , Wakurugenzi, Wataalamu wa kilimo pamoja na wadau wa kilimo wa Mkoa wa Dodoma.

#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.