• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DODOMA YAFANYA TATHMINI YA MICHEZO YA UMITAMSHA NA UMISSETA

Imetumwa : July 22nd, 2025

Na; Happiness E. Chindiye

      Habari - Dodoma RS

Katibu  Tawala Msaidizi Sekta ya Elimu  Mwl. Vicent Kayombo Julai 21,2025 amekutana na Maafisa Elimu Halmashauri, Maafisa Elimu Kata na Maafisa Michezo wa Halmashauri zote za Mkoa huu kwa lengo la kufanya tathmini ya michezo ya Umoja wa Mchezo na Taaluma kwa Shule za Msingi Tanzania (UMITASHUMTA)  na Umoja wa Mchezo ya Shule Sekondari (UMISSETA).

Akizungumza kwenye kikao hicho kilichofanyika kwenye ukumbi wa Maria de Matias amewataka maafisa hao kuwa mstari wa mbele kuhakikisha mashindano hayo katika Mkoa  wa huu  unakuwa wa kitofauti na kuwa  kinara kwenye mashindano hayo.

“Kufika kwenu katika kikao hiki cha tathmini si kwa bahati mbaya, ninyi nyote ndio kisima cha maarifa ya mafanikio ya michezo kwenye Mkoa wetu. Natamani nyote mliopo hapa kila mmoja adhamirie kwenda kufanya jambo zuri litakaloacha alama mahali alipo kwenye sekta hii ya michezo.

Kila mtu uone michezo ya mwaka 2026 ya UMITASHUMTA na UMISSETA ina siku chache kabla ya kuanza ili usukumwe kuweka mikakati yako binafsi katika kufanya jambo litakalotufanya wote tutakapo kutana tena mwakani tukupongeze kwa kutekeleza maazimio ya kikao hiki kwa uzalendo.

“Kuna usemi wa Kiswahili unasema ‘’palipo na nia pana njia’’ nia ipo ndio sababu ya sisi kukutana leo mahali hapa, jukumu lenu kila mmoja ni kuonesha njia ilipo, kama ipo kwenye soka kafanye jambo kwenye soka, kama ipo kwenye mpira wa goli kafanye jambo kwenye goli, kama ipo kwenye riadha kafanye jambo kwenye riadha kadhalika na michezo mingine yote tunayoshiriki ngazi ya Taifa, kila mmoja ajipime aone kwake njia ipo eneo gani.

" Tunaowajibu wa kufanikisha Mkoa wetu kwa sababu sisi ndio wataalamu lazima tuufanye mkoa wa dodoma uwe katika sura ya kitofauti" - Ameeleza Mwl. Kayombo

Aidha Afisa Elimu huyo amewapongeza timu hiyo kwa jitihada zote walizofanya kwenye mashindano hayo ya mwaka huu na kwa ushindi kwenye mchezo iliyofanya vizuri na kuwatia moyo kuongeza juhudi kwa ajili ya mashindano yajayo.

Kikao cha tathmini katika eneo la mchezo kimeibua ari ya maafisa hao kutoa maoni yao na kuweka  maazimio ya pamoja ambayo yatasaidia yatasababisha sekta hiyo kufanikiwa kwa kiwango kizuri kwenye mashindano ya mwaka 2026.


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajiwangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MRADI WA ‘KOFFI’ WATOA DOLA BILIONI 2.455 KUBORESHA HUDUMA ZA UZAZI NA MTOTO DODOMA

    August 21, 2025
  • WANANCHI NA WADAU WAASWA KUCHAGIZA UTALII - DODOMA

    August 21, 2025
  • WADAU WAASWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA JAMII DHIDI YA MAJANGA

    August 19, 2025
  • WAFANYABIASHARA WA MKOA WA DODOMA WATANGAZIWA FURSA ZA BIASHARA NCHINI INDONESIA

    August 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.