• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DODOMA YAJIANDAA KWA TUKIO KUBWA LA ZIARA YA MABALOZI MEI 27

Imetumwa : May 23rd, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amefanya Mkutano na Waandishi wa Habari Mei 23, 2025 kwenye ukumbi wa Ofisi yake Jijini Dodoma ukiwa na lengo la kuutangazia Umma juu ya tukio kubwa la Kimataifa la ziara ya Mabalozi Mkoani hapa.Mabalozi hao ni wale wanaoiwakilisha Tanzania kwenye nchi mbalimbali Duniani,na wanaoziwakilisha Nchi zao hapa Nchini.

Tukio hilo litakalofanyika siku ya Jumanne Mei 27, linatarajiwa kuwa la kipekee ambapo Mhe. Senyamule ameelezea dhumuni hasa la ugeni huo.

“Dhumuni la kwanza ni kuwaeleza Waheshimiwa Mabalozi mambo yaliyopo katika Mkoa wa Dodoma na kuwa tuna huduma zote, wakiishi hapa; afya, elimu, miundombinu, maji, umeme na vitu vingine ambavyo vingemfanya mtu afurahie kukaa mahali, tunataka tuwaoneshe kuwa Dodoma huduma hizo tayari zipo na tunatamani waje sasa”.

Aidha, Mhe. Senyamule amesema kuwa Dodoma ina vivutio vingi vya utalii na fursa za uwekezaji hivyo anatamani watu kutoka nchi mbalimbali duniani,zikiwemo  ambazo mabalozi hao wanatoka,waje kuwekeza,kadhalika kuwaonesha kuwa Dodoma ni mahali sahihi na kuna fursa ya kufurahia utalii kama yalivyo maeneo mbalimbali ya nchi yetu.

Kadhalika, Mkuu huyo wa Mkoa amebainisha kuwa wanatamani Dodoma iwe na majina ya nchi za Kimataifa katika Mitaa kwani wanatamani Dunia ihamie Dodoma kwa kuwaambia Mabalozi fursa hiyo ambayo itawawezesha kufahamu maeneo kwa majina ya nchi zao kama vile mtaa wa Wachina, Wahindi na mingineyo ipatikane Dodoma.

Jambo jingine lililokusudiwa kwenye ziara hiyo ni kuwafahamisha wageni hao kuwa Dodoma ina Wilaya saba na Halmashauri nane ambazo zote zinahitaji kupata Miji rafiki kutoka katika nchi zao kwa ajili ya kubadilisha na uzoefu katika sekta mbalimbali ili kukwamua uchumi wa Mkoa kwa kushirikiana na watu wengine.

Ujio huo unatarajiwa kuhusisha kikao ambacho kitawaonesha na kuwapitisha mambo yote ya Mkoa wa Dodoma, baada ya hapo watatoka na kwenda kujionea mambo hayo wakianzia Hospitali ya Benjamin Mkapa, Mji wa Serikali Mtumba na kuishia Kiwanja cha Ndege Msalato.

Ziara hiyo imeandaliwa kwa kutambua mchango wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye amejenga mahusiano mazuri na nchi zote Duniani zinazowafanya wafurahie kuja Tanzania na haya yote wamekua wakiyafanya katika nchi mbalimbali hivyo sasa ni zamu ya Dodoma.

Kaulimbiu: “Dodoma ipo Tayari kwa Ajili yenu”


#dodomawearereadyforyou

#takedodomatotheworldandbringtheworldtododoma

#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MMUYA AHIMIZA UDHIBITI VIFO VYA MAMA NA MTOTO

    May 26, 2025
  • UHAKIKI ANUANI ZA MAKAZI KUANZA MEI 28 DODOMA

    May 26, 2025
  • WAWEKEZAJI WA VIWANDA KUTOKA DUBAI WABISHA HODI DODOMA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI KUTOKA TUME YA MADINI WAMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.