• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DODOMA YAJIPANGA KISAWASAWA KUPANDISHA UFAULU 2025

Imetumwa : December 12th, 2024

Na. Sizah Kangalawe

Habari- Dodoma Rs

Mkoa wa Dodoma umeendelea  kupandisha viwango vya  ufaulu wa ngazi ya Elimu ya Msingi kwa 0.84%  kati ya mwaka 2022 - 2024.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati akiwahutubia wataalam na wadau wa Elimu wa Mkoa, walioshiriki kikao kazi cha siku tatu cha tathmin ya Elimu kwa mwaka 2024 na kuandaa mipango mikakati ya kupandisha ufaulu kwa mwaka wa masomo 2025.

kikao kazi hicho kimefanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Ualimu Bustani kilichopo Wilayani Kondoa.

 "Viwango vya ufaulu vinaendelea kuongezeka, mathalani mwaka 2022 ulikuwa 83.01%, 2023 ukafikia 87.05%, na Mwaka 2024  87.89% sawa na ongezeko la 0.84% kwa Elimu ya Msingi.

"Mkoa Umeongeza ufaulu kwa 0.84 kwa mtihani wa Darasa la Saba, bado tunasubiri matokeo ya upimaji wa darasa la Nne, Kidato cha Pili na matokeo ya mtihani wa Kidato cha Nne 2024, tuombe Mungu atujalie ufaulu upande", Mhe Senyamule

Aidha Mhe.Senyamule amekiri kuwepo kwa hali nzuri ya utoaji wa chakula shuleni katika shule za Msingi na Sekondari kwani hadi kufikia Novemba 2024 wanafunzi 598,376 kati ya wanafunzi 731,936 ikiwa ni sawa na 81.08% wa Elimu ya Awali, Msingi na Sekondari walipatiwa chakula cha mchana Shuleni.

Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Dodoma Mwl.Vicent Kayombo amesema Seksheni ya Elimu Mkoa imejipanga kuutangaza vyema Mkoa kupitia utoaji wa Elimu.

"Sisi wataalamu wa Elimu Mkoa wa Dodoma katika Mkoa huu tumejipanga kuufanya Mkoa ujitangaze kupitia Mipango inayotekelezeka ya usimamizi wa Elimu inayotoa matokeo chanya na hivyo kuutangaza Mkoa Kupitia Utoaji wa Elimu bora kwa watoto wa Mkoa huu.

"Uwepo wetu hapa una lengo la kuhakikisha tunainua ubora wa Elimu yetu na tunaongeza ufaulu kwa mitihani yote ya Taifa tunayofanya, kwa ngazi zote za upimaji wa kidato cha pili,cha Nne na Sita,Upimaji wa Kitaifa wa Darasa la Nne pamoja na mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba.Naamini wazi furaha ya kila mmoja ni kuiona Dodoma ikiwa kinara kwenye mitihani hii na hapa ndipo tunapojipima waziwazi", Mwl. Kayombo

Kikao kazi hicho kimewajumuisha Maafisa Elimu ngazi ya Wilaya na Mkoa, Wathibiti Ubora wa Shule,CWT Dodoma, Shule Bora, pamoja na wadau wengine mbalimbali wa Sekta ya Elimu.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.