• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI YA AWAMU YA SITA IMETATUA KWA KIASI KIKUBWA KERO ZA WALIMU NCHINI

Imetumwa : October 18th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Kero mbalimbali za Walimu nchini ikiwemo kupandishwa vyeo na nyongeza ya mishahara, zimeendelea kutatuliwa kwa kiasi kikubwa na Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan hali ambayo imeleta tija kwa maisha ya Walimu sambamba na uboreshaji wa miundombinu ya Utumishi.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati akizungumza na Viongozi wa Walimu kutoka Mikoa ya Kanda za Kati na Kaskazini  kwenye Mkutano Mkuu wa ujirani mwema unaofanyika kwenye ukumbi wa Klabu ya Kilimani Jijini hapa kwa siku mbili kuanzia leo Oktoba 18 hadi 19, 2025.

“Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan, imeendelea kutatua kero za Walimu ikiwemo kupandishwa vyeo, nyongeza ya mshahara kila mwaka ambayo imeleta tija, kubadilishwa miundombinu ya Utumishi na kulipa madeni mbalimbali ikiwemo madeni ya likizo, matibabu, uhamisho, fedha za kufunga mizigo kwa Wastaafu.”

Aidha, Rais wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Dkt. Suleiman Ikomba, amesema Uongozi mpya wa Chama hicho una matamanio ya Walimu kuonekana ni Kioo cha jamii hivyo, ndani ya miaka mitano ya uongozi wake, wapo tayari kushirikiana na Serikali na jamii nzima ya Tanzania ili kuiletea maendeleo nchi na kufikia matamanio hayo.

Katika Risala iliyosomwa na Mwalimu Asha Juma, viongozi hao wamependekeza Serikali kuepuka madeni ya Walimu yasiyo ya mishahara kwa kuingiza fedha za likizo moja kwa moja kwenye Akaunti  za Benki za wahusika sambamba na kuendelea kutoa mafunzo ya matumizi ya Mifumo ya Kiutumishi ili kutatua changamoto inayowakabili baadhi yao.

 Umoja wa Walimu wa Kanda ya Kati na Kaskazini unaojumuisha Walimu kutoka Mikoa sita ya Arusha, Dodoma, Tanga, Kilimanjaro, Manyara na Singida, ulianzishwa 2022 ukiwa na lengo la kuwaunganisha Walimu hao ili wabadilishane uzoefu na kutatua changamoto zinazowakabili ili kutekeleza kaulimbiu ya CWT ambayo ni “Wajibu na Haki”.


#DodomaFahariyaWatanzania

#KuraYakoHakiYakoJitokezeKupigakura

#NimejiandikishaNitapigaKura

#UmejiandikishaKapigeKura

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • SERIKALI YA AWAMU YA SITA IMETATUA KWA KIASI KIKUBWA KERO ZA WALIMU NCHINI

    October 18, 2025
  • DODOMA WAFANYA MAZOEZI YA AMANI KULIOMBEA TAIFA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29,2025

    October 18, 2025
  • UJIO WA MKANDARASI MPYA WA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA KULETA FURSA ZA KIUCHUMI KWA WANANCHI

    October 13, 2025
  • “ TUTAYAENZI NA KUYATANGAZA MEMA ANAYOYAFANYA MHE. RAIS “ RC SENYAMULE

    October 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.