• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DODOMA WAFANYA MAZOEZI YA AMANI KULIOMBEA TAIFA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29,2025

Imetumwa : October 18th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Ukosefu wa Amani mahali popote unatajwa kujenga chuki, kuondoa mapatano, kupoteza haki kwa baadhi ya watu na kuchelewesha maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla. Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa mazoezi ya kuhamasisha Amani wakati zikisalia siku chache Taifa kuingia kwenye uchaguzi Mkuu Oktoba 29, 2025.

Mazoezi ya kuhamasisha Amani yaliyoandaliwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, yamefanyika leo Oktoba 18, 2025 kwa matembezi yaliyolenga kuimarisha viungo vya mwili yaliyoanzia kwenye Jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hadi viwanja vya Nyerere (Nyerere Squre) katikati ya Jiji.

Akizungumza na makundi mbalimbali ya kijamii yalijitokeza kushiriki mazoezi hayo yaliyoambatana na maombi kutoka kwa viongozi wa Madhehebu ya Dini yanayopatikana Mkoa wa Dodoma kuliombea Taifa, Mhe. Senyamule amesema;

“Tunajua, ukosefu wa Amani mahali popote unajenga chuki, unaondoa mapatano, unapoteza haki kwa baadhi ya watu, lakini pia unachelewesha maendeleo. Sisi Tanzania na hata maeneo mengi Duniani, tumeona nchi ambazo zimepoteza Amani, kuja kuirudisha Amani ile si jambo rahisi sana na wakati fulani inachukua karne na miongo”.

Kadhalika, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri, amesema kuwa kila aliyeshiriki mazoezi hayo ni Balozi wa kuhamasisha Amani kwa nafasi na mazingira yake kwani kuzungumzia Tunu za Amani ni jambo la kiucha Mungu kutokana na vitabu vya Dini pia kusisitiza Amani wakati wote.

Hata hivyo, Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Dkt. Khatibu Kazungu, amesema mazoezi hayo ni moja ya ajenda zinazohubiriwa na Mhe. Senyamule kila wakati zikilenga kuhakikisha Mkoa unakua mahali salama, penye Amani na wananchi wake wanafanya shughuli zao za kiuchumi na maendeleo bila ghasia za aina yeyote.

Mbali na Viongozi wa Madhehebu ya Dini, makundi ya kijamii yaliyoshiriki mazoezi hayo ni Maafisa usafirishaji wa Bajaji na Pikipiki, Watu wenye ulemavu, Wakulima, Umoja wa Wanawake Machinga, Machifu, Wanawake na Samia, Vikundi vya Jogging, Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania, Watumishi wa Idara Mbalimbali na Baraza la Wazee

Sanjari na mazoezi hayo yaliyoongozwa na Kaulimbiu; ‘‘Nitailinda Amani ya Nchi Yangu, Kabla, Wakati na Baada ya Uchaguzi’’ pia imeandaliwa Kambi maalumu ya Uchunguzi na Matibabu ya Kibingwa ya Magonjwa ya Moyo, Macho, Figo, Saratani na Selimundu inayoendeshwa na Madaktari Bingwa kutoka Hospitali ya Kanda ya Benjamini Mkapa.


#DodomaFahariyaWatanzania

#KuraYakoHakiYakoJitokezeKupigakura

#NimejiandikishaNitapigaKura

#UmejiandikishaKapigeKura

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • SERIKALI YA AWAMU YA SITA IMETATUA KWA KIASI KIKUBWA KERO ZA WALIMU NCHINI

    October 18, 2025
  • DODOMA WAFANYA MAZOEZI YA AMANI KULIOMBEA TAIFA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU OKTOBA 29,2025

    October 18, 2025
  • UJIO WA MKANDARASI MPYA WA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA KULETA FURSA ZA KIUCHUMI KWA WANANCHI

    October 13, 2025
  • “ TUTAYAENZI NA KUYATANGAZA MEMA ANAYOYAFANYA MHE. RAIS “ RC SENYAMULE

    October 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.