• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Katibu Mkuu Chama Tawala Burundi,Apongeza Uwekezaji Kiwanda cha Mbolea -Dodoma

Imetumwa : July 12th, 2022

Katibu Mkuu Chama Tawala Nchini Burundi CNDD – FDD   Mhe.Reverien Ndikuriyo, akiwa ameambatana na  Balozi wa Burundi nchini Tanzania Mhe. Gervas Abayeho pamoja na  Mshauri wa Katibu Mkuu CNDD-FDD Mhe. Said Kibeya , hivi karibuni wametembelea makao Makuu ya Nchi Dodoma, ili kujionea  na kujifunza shughuli mbalimbali zinazofanyika  katika Makao ya  nchi.

Katika ziara hiyo ujumbe huo umeambatana na mwenyeji wao Naibu Katibu Mkuu Chama cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Mhe. Christina Mndeme pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka. Aidha ujumbe huo  umetembelea Chuo Kikuu cha UDOM, Kituo cha Mabasi cha Job Ndugai, Kiwanda cha Mbolea  cha Intracom pamoja na Machinga Complex.

Wakiwa katika kiwanda cha mbolea cha Itracom Fertilizers Ltd wameelezwa kuwa kiwanda hicho kitakuwa na Majengo ya Viwanda/‘Plant Line’ 3, Maghala 6, Maabara, Gereji kwa ajili ya Ukarabati wa Magari, Jengo la Utawala, Mgahawa na zahanati.  Inakadiriwa kwamba kila Plant line itakuwa inazalisha tani 200,000 za mbolea kwa mwaka, wakati  chokaa/limestone itakayozalishwa ni tani 300,000 kwa mwaka.Aidha wageni hao walifahamishwa kuwa jengo la kwanza  la Kiwanda limeshakamilika .

Kiwanda cha mbolea cha Intracom Fertilizers Ltd, kitazalisha Mbolea aina ya ‘Organo mineral fertilizer’- mbolea ambayo ni mchaganyiko  wa mbolea ya asili ya samadi na mbolea  za kiwandani. Kitu cha pekee kuhusiana na mboela hiyo, ni kwamba mbolea hiyo inataja kiwango cha mbolea kinachohitajiwa kwa kila mmea na kama matokeo  matumizi ya mbolea hiyo yatafanya udogo uendelee kuwa na rutuba.

Akizungumzia manufaa za mbole hiyo Meneja wa Kiwanda hicho amesema  kuwa kiwanda hicho kitazalisha mbolea za aina tatu ambazo ni mbolea ya kupandia, mbolea ya  kukuzia na mbolea ya kunenepesha. Aidha upatikanaji wa mbolea ya Intracom ni wenye faida kwa Watanzania kwani  ni wa bei nafuu sababu ya upungufu wa gharama za usafirishaji, inakaa kwenye udongo sababu ina vimelea vya asili na inapatikana kwa bei nafuu kwa sababu inapatikana hapa hapa nchini.

Akizungumza Naibu Katibu Mkuu CCM Tanzania Bara Mhe.Christina Mdeme, amepongeza uwepo wa kiwanda hicho kwani utatoa ajira kwa Watanzania, mbolea inayozalishwa ni rafiki, ni chanzo cha mapato kwa  Nchi na Halmashauri. Aidha Mhe. Mndeme amewataka  Wafugaji  kutunza samadi badala ya kuichoma kwani kinyesi cha wanyama sasa ni mali. “Tuongeze ufugaji na tuitunze mbolea yetu, tutumie fursa kuhakikisha tunatunza kinyesi  cha wanyama na kukiwasilisha katika hiki kiwanda.Wakulima tutumie mbolea rafiki toka hapa’’ Amesisitiza  Mhe. Mndeme.

Vilevile Mhe. Mdeme amempongeza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Mtaka kwa kusimamia vyema uwekezaji huu mkubwa na kutoa kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa Sports Academy.

Nae Katibu Mkuu chama Tawala nchini Buirundi CNDD-FDD Mhe. Mhe.Reverien Ndikuriyo, amepongeza ujenzi wa kiwanda cha Intracom Fertilizers,”nimevutiwa sana kuona vifaa vyote vya mashine na ujenzi vinafungwa na vijana wa Kitanzania, hii inaonyesha uwezo mkubwa na nguvu kazi ya Kitanzania, pia inathibitisha wazi kwamba Tanzania ipo salama.Nitoe pongezi nyingi sana kwa mwekezaji , kwani uwekezaji huu unazalisha ajira kwa vijana, wakulima na wafugaji. Pongezi kwa mbolea ya viwango”.Amesema Mhe. Ndikuriyo.

Mhe.Ndekuriyo ameahidi kujenga shule ya Michezo / ‘Sports academy’ mara baada ya kumaliza ujenzi wa Sport Academy nchini Burundi. Kusudi la Sports Academy ni kuwaandaa Vijana kucheza mpira wa kimataifa.Aidha niwashukuru sana kwani zira hii imekuwa nzuri sana na yenye mafanikio. Nchini Burudi tuna Kiwandacha mbolea kama hikiambacho kilianza miaka 6 iliyopita na kinazalisha mbolea tani 150,000 kwa mwaka.

Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka ameeleza kuwa Kiwanda cha Mbolea cha Intracome Fertilizers kilichopo eneo la Nala Jijini Dodoma, ni kiwanda kikubwa cha mbolea nchini Tanzania ,huku mwekezaji wake Bw. Bwn. Adrian Ndikachika akiwa ametokea  nchini Burundi. Kiwanda hiki kimejengwa kwa gharama ya Tsh.480 bil na kinatarajia kuzalisha ajira kwa watanzania 3000. 

Aidha Mhe. Mtaka amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kuwezesha uwekezaji nchini na kwa kuwajali makundi yote ya Watanzania. Mhe. Mtaka amemhakikishia Mhe, Ndikuriyo kwamba, uwanja wa kujenga Sports Academy Dodoma utapatikana na hivyo akimaliza mradi huo Burundi asisite kuja kuwekeza  Makao Makuu ya Nchi Dodoma. MWISHO.

 

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.