• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MRADI WA ‘KOFFI’ WATOA DOLA BILIONI 2.455 KUBORESHA HUDUMA ZA UZAZI NA MTOTO DODOMA

Imetumwa : August 21st, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Mkoa wa Dodoma umepokea kiasi cha Dola Milioni 2.455 ambazo zinakadiriwa kuwa sawa na Shilingi Bilioni 5.524 katika kipindi cha miaka minne ya Mradi wa uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na Mtoto unaofadhiliwa na Serikali ya Korea kupitia Taasisi ya Kimataifa ya kuboresha Afya ‘Korea Foundation for International Healthcare’ (KOFIH).

Fedha hizo zinatajwa kutumika kuboresha mazingira ya utoaji huduma za Afya kwenye vituo vya Mradi huo ambao unatekelezwa katika Wilaya Mbili za Mkoa huu ambazo ni Kongwa na Mpwapwa.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amebainisha hayo alipokua anafungua kikao cha Tathmini ya Mradi wa Uboreshaji wa Huduma za afya ya uzazi na Mtoto chini ya KOFIH kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano ndani ya Hoteli ya Rafiki Jijini Dodoma leo Agosti 21, 2025

“Kwa kipindi cha miaka minne, Mkoa umepokea Dola takribani Milioni 2.455 ambazo zinakadiriwa kuwa sawa na Shilingi Bilioni 5.524 fedha hizi zimetumika kwa ajili ya mafunzo kwa Watumishi, ujenzi na ukarabati wa majengo 17 katika vituo vya Mradi, ununuzi wa vifaa tiba, magari mawili ya wagonjwa sambamba na majenereta 7”.

Aidha, Mwakilishi Mkaazi wa KOFIH Bw. Gyeongloae Seo, amesema lengo hasa la Mradi ni kupunguza vifo vitokanavyo na Uzazi katika Mkoa wa Dodoma hivyo, wanaangalia kupanua wigo kuelekea kwenye Wilaya nyingine za Mkoa huu ili malengo ya Mradi yaweze kufikiwa kwa ukubwa na kuleta tija kwa Serikali na jamii kwa ujumla.

Hata hivyo, Mwakilishi kutoka Wizara ya Afya ambaye ni Mkuu wa Program ya Uzazi Salama Dr. Phineas Sospeter amesema lengo la Serikali kupitia Wizara yake ni kupunguza vifo vya uzazi na mtoto mchanga hivyo, wanatoa ushirikiano kwa Mradi huo muhimu kwani unachangia katika kufikia malengo yao.

Wilaya ya Kongwa imetenga Shiligi Milioni 492.3 (2025/26) kwa ajili ya shughuli za utoaji Elimu ya uzazi kwa jamii, ujenzi wa njia za wagonjwa kwenye vituo viwili, usimikaji wa Mifumo ya Oksijeni kwenye jengo la Wazazi, ununuzi wa vifaa tiba pamoja na ununuzi wa gari ya kubebea wagonjwa katika vituo vinne vya Mradi (Hospitali ya Wilaya, vituo vya afya Chamkoroma, Mkoka na Kibaigwa).

Nayo Wilaya ya Mpwapwa, imetenga bajeti ya Shilingi Milioni 556.5 (2025/26) kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli za usambazaji wa vifaa tiba, utoaji elimu ya uzazi kwa jamii, ununuzi wa majenereta 02 na gari 01 kwa ajili ya kurahisisha shughuli za utoaji huduma kwenye vituo 08 vya Mradi ambavyo ni Hospitali ya Wilaya, Vituo vya Afya Ipera, Mima, Kibakwe, Pwaga, Rudi, Zahanati za Winza na Mlunduzi.

Mradi wa Uboreshaji wa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto chini ya KOFIH unatekelezwa katika Wilaya mbili za Mkoa wa Dodoma ambapo ulianza utekelezaji wake 2021, unatarajiwa kutamatika 2026 ambapo kupitia Mradi huo, Vituo vilivyochaguliwa vimenufaika na uboreshaji wa mazingira ya utoaji huduma za afya kwa wananchi.



 #dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MRADI WA ‘KOFFI’ WATOA DOLA BILIONI 2.455 KUBORESHA HUDUMA ZA UZAZI NA MTOTO DODOMA

    August 21, 2025
  • WANANCHI NA WADAU WAASWA KUCHAGIZA UTALII - DODOMA

    August 21, 2025
  • WADAU WAASWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA JAMII DHIDI YA MAJANGA

    August 19, 2025
  • WAFANYABIASHARA WA MKOA WA DODOMA WATANGAZIWA FURSA ZA BIASHARA NCHINI INDONESIA

    August 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.