• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KUMBUKENI THAMANI YA UHAI WA BINADAMU; RAS MMUYA

Imetumwa : January 13th, 2025

Na. Sizah Kangalawe

Habari- Dodoma Rs.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K.Mmuya wakati akifungua kikao kazi cha kupanga namna bora harakishi na jumuishi ya kuwatafuta na kuwaibua wagonjwa wa kifua kikuu, kikao ambacho kimewajumuisha Waganga Wakuu wa Wilaya, Waratibu wa Kifua Kikuu na UKIMWI, Waratibu wa kifua kikuu na Ukoma pamoja na Wataalamu wa Maabara kutoka halmashauri 7 za Mkoa wa Dodoma.


Kikao hicho kimefanyika Januari 13/2025  katika ukumbi wa Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali Jijini Dodoma.

Akizungumza wakati akifungua kikao hicho Mmuya amesema " Wote tunaujua ugonjwa wa kifua kikuu, usipoweza kumtambua mgonjwa mmoja, ana uwezo wa kuwaambukiza watu 15 hadi 20  kwa mwaka mmoja Ndio sababu tunasisitiza wagonjwa watambuliwe mapema.Leo mmekutana wataalamu hapa, jadilianeni mtoke na mbinu zitakazowawezesha kwenda kuwatambua na kuwaibua wagonjwa  1,930 ndani ya muda uliowekwa.

 Aidha RAS Mmuya ametaja takwimu za ugonjwa huo Kidunia na Kitaifa ambapo amesema " kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani, mwaka 2023 kulikuwa na wagonjwa Milioni 10. 8, kati ya hao Wagonjwa Milioni 1.25 walifariki, Mwaka 2024  Tanzania ilikuwa na wagonjwa 122,000 ambapo wagonjwa 18,400 walifariki.

"Idadi hiyo ya vifo ni kubwa sana, hii si sawa, nguvu kazi ya Taifa imepotea na kilichoniuma  zaidi ni kwamba tuna uwezo wa kuokoa maisha yao kwa sababu dawa za kutibu zipo.

"Mhe. Rais anawekeza fedha nyingi sana kwenye kujenga nguvu kazi kuleta tija kwenye sekta ya Afya, na sisi tumuunge mkono kwa kufanya kazi kwa bidii ili Taifa liweze kupata matokeo tarajiwa. Kumbukeni thamani ya uhai wa binadamu", Amesema Mmuya

Katibu Tawala huyo ameongeza  kuwa ni muhimu kufahamu takwimu za ugonjwa, ili kuongeza jitihada za  kukabiliana nao.

Kikao hicho maalum ni utekelezaji wa mpango harakishi wa kuibua wagonjwa wa kifua kikuu katika halmashauri 76 za mikoa 9  uliozinduliwa Januari 06,2025 na Waziri wa Afya Mhe. Jenista Mhagama katika kituo cha Afya  Chamwino, kilichopo wilayani Chamwino wakati akikabidhi mashine za utambuzi na ugunduzi wa Ugonjwa wa kifua kikuu.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.