• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

KUONGEZA UZALISHAJI WA ALIZETI DODOMA; SENYAMULE ATAKA MKAKATI WA PAMOJA

Imetumwa : September 16th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Viongozi wa Halmashauri za Mkoa wa Dodoma hususan maeneo yanayolima zao la Alizeti kwa wingi, wametakiwa kuhakikisha Wakulima wanalima zao hilo pekee katika msimu mmoja wa kilimo ili uwepo uhakika wa malighafi hiyo muhimu kwa utengenezaji wa Mafuta ya kupikia inakidhi mahitaji ya viwanda vya mafuta ya Alizeti kwa mwaka mzima.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule Septemba 16, 2025 alipotembelea Kiwanda cha kutengeneza Mafuta ya Alizeti ‘Cemex Ventures Limited’ kilichopo eneo la Viwanda Kizota Jijini Dodoma wakati wa ziara ya kikazi kukagua miradi ya maendeleo sanjari na Viwanda vinavyozalisha bidhaa mbalimbali.

“Tukae pamoja tuone namna tunavyoweza kuongeza uzalishaji wa Alizeti kwa kuhakikisha lazima msimu mmoja Wakulima walime Alizeti pekee ili kukidhi mahitaji ya Alizeti kwa Wawekezaji kwenye maeneo yote yaliyowekewa miundombinu ya umwagiliaji ambapo kilimo kitakua kila wakati bila kutegemea mvua za msimu”

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri, amekipongeza Kiwanda hicho kwa kupanua matumizi ya teknolojia za kisasa ambayo yanaongeza ufanisi katika uzalishaji wa mafuta ya Alizeti na kuongeza kuwa Viongozi wa Mkoa wana wajibu wa kuhakikisha malighafi ya kutosha inapatikana mwaka mzima kiwandani hapo.

Mbali na Kiwanda hicho, Mhe. Senyamule katika ziara yake pia ametembelea Kiwanda cha uzalishaji wa Mabati (TAISHAN) kinachopatikana eneo la Viwanda Kizota ambapo kiwanda hicho kinazalisha bidhaa za Mabati ya aina tofauti tofauti na kwa gharama nafuu ambazo mwanachi wa kawaida anaweza kuzimudu.

Akiwa Kiwandani hapo, Mhe. Senyamule Senyamule amesema kupitia Kiwanda hivyo, Utashi wa kulipendezesha Jiji la Dodoma kupitia rangi za Mabati unawezekana kwani kutokana na taratibu za Mipango Miji, kila eneo lina rangi ya Bati ambayo inarahisisha utambuzi wake hata kwa wageni wanaoingia kila uchao Jijini hapa.

Vile vile, ziara hiyo ilifika kwenye kiwanda cha utengenezaji wa viatu kinachojulikana kama ‘Jin’kui Shoes Ltd’ chini ya mwekezaji kutoka China kinachozalisha aina tofauti za Raba ambapo Mhe. Senyamule ametoa maelekezo kwa Maafisa Biashara wa Jiji na wa Mkoa, kuhakikisha kiwanda hicho kinapata soko la uhakika ndani na nje ya Mkoa.

Awali, ziara hiyo ilianza kwa ukaguzi wa miradi ya maendeleo ambayo ni ujenzi wa Maabara mbili za Sayansi, moja katika kila shule ambazo ni Sekondari ya Kisasa na Sekondari ya Kizota ambapo Sekondari ya Kisasa ilipokea Shilingi Milioni 20 huku Sekondari ya Kizota ikipokea Milioni 30.Utekelezaji wa miradi hiyo unaendelea huku ikitarajiwa kuongeza ufanisi wa kujifunzia kwa Wanafunzi pindi itakapokamilika Oktoba, 2025.

 #dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KUONGEZA UZALISHAJI WA ALIZETI DODOMA; SENYAMULE ATAKA MKAKATI WA PAMOJA

    September 16, 2025
  • RAS DKT. KAZUNGU KUJA NA MKAKATI WA KUKUZA UCHUMI WA DODOMA

    September 16, 2025
  • SERIKALI YATEKELEZA MIRADI YENYE MANUFAA KWA WANANCHI WA WILAYA YA CHAMWINO

    September 15, 2025
  • RAS DKT. KAZUNGU AWATAKA WATUMISHI WA SERIKALI KUFANYA KAZI KWA WELEDI , JUHUDI NA MAARIFA

    September 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.