• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

“MHE. RAIS AMEFUNGUA NCHI, MWAMKO WA WATU KUJUA ITIFAKI, UMEONGEZEKA” - RC SENYAMULE

Imetumwa : January 26th, 2025

Na. Sophia Remmy

Dodoma RS - Habari

Mkuu wa  Mkoa wa Dodoma,mheshimiwa Rosemary  Senyamule amesema kuwa mwamko wa watu wengi kujifunza  masuala ya itifaki umetokana na utashi wa Mhe. Rais katika masuala ya Diplomasia pamoja kazi kubwa anazozifanya .

Mhe. Senyamule ameyasema hayo  leo Januari 26,2025, wakati akifunga mafunzo ya siku 3 ya  Itifaki ya Diplomasia na ustaarabu yaliyoandaliwa na taasisi binafsi ya  'Protocol Service Team'(PST)  kwenye ukumbi wa Kapteni John Komba uliopo Jakwaya Kikwete Conversation Center jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa hotuba yake Mhe. Senyamule ameeleza umuhimu wa mafunzo hayo kwa Wananchi, ambapo amesema kuwa unatokana na mabadiliko yanayoendelea kutokea  Nchini.

" Kipekee kabisa nichukue fursa hii kumpongeza  Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Daktari Samia Suluhu Hassan,tunapompongeza Mhe. Rais kila wakati, wananchi wengine hawajui ni kwa nini tunampongeza, tunampongeza  si kwa sababu tunataka tu   kusema,tunampongeza kwa sababu na yeye kuna mambo ameyafanya.

Mimi nilipokuwa naendelea kutafakari,kwa nini mwamko wa mambo ya itifaki  umekuwa mkubwa sasa,nikaona kuna kitu amekifanya, kimepelekea mahitaji ya watu wa kujua itifaki kuwa mengi.

Yeye alipofungua Nchi,sisi tu,mfano wa hapa Dodoma,watu wanaokuja,mimi nikikaa ofisini kila siku,kila wiki napokea Mabalozi wawili,watatu,napokea mikutano ya kutosha,naona hivyo Arusha,naona hivyo          Dar es Salaam,na Mikoa mingine pia naona.Sasa wote tukiwa na mikutano,tutahitaji  watu wa kutuongoza,watu wa kuongoza wageni,kwa hiyo yeye alipofungua Nchi,amefungua kwa namna ambayo yeye alisema,lakini 'impact' yake imetugusa hata sisi ambao tunahitaji watu wa kuongoza mikutano,na taratibu nyingine ziende vizuri.Amesema Mhe. Senyamule

Mhe. Senyamule ameongeza kusema kuwa baada ya historia ya  miaka mingi Tanzania inapokea Marais wa Nchi za Afrika 25,Mawaziri wa Fedha na Mawaziri wa nishati 60,na kwamba hilo sio jambo dogo, ni kutokana na kazi anayoifanya Mhe Rais ambayo Dunia inaiona.

Katika miaka ya karibuni, tumeshuhudia kuimarika kwa kiasi kikubwa kwa uhusiano wa Kimataifa kati ya Nchi yetu na Mataifa mengi Duniani,hayo yote ni matunda ya jitihada za Rais wetu kuimarisha demokrasia na kuendesha Nchi katika misingi aliyojiwekea ya R 4.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.