• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MKOA WA DODOMA KUJA NA MPANGO MKAKATI WA KUKUZA NA KUTANGAZA UTALII WA NDANI

Imetumwa : July 11th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Utalii unatajwa kuwa na athari chanya za kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja na Mkoa kwa ujumla pale unapotumika kimkakati. Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amebainisha hayo alipokua akifungua kikao Maalumu cha Maandalizi ya uzinduzi wa Kitabu cha Mpango Mkakati wa Kukuza na Kutangaza Utalii wa Mkoa huu.

Kikao hicho kimewahusisha Wadau wa utalii kutoka sekta mbalimbali waliokutana kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jijini hapa Julai 11, 2025 lengo likiwa ni kupitia Mpango Mkakati ulioandaliwa sambamba na kuunda Kamati itakayoshughulikia kwa karibu ufanikishaji wa shughuli hiyo.

“Utalii una athari nyingi za kiuchumi kama ukiwa nao maana utakuza uchumi wa mtu mmoja mmoja lakini pia wa Mkoa. Dodoma tunatamani tuwe ‘hub’ ya utalii kwa sababu tunafikika kila upande wa nchi ya Tanzania hata kama vivutio vya utalii havipo Dodoma tunataka iwe active kwenye suala la utalii”. Mhe. Senyamule.

Akizungumza katika kikao hicho, Katibu Tawala Msaidizi Sekta za Viwanda, Biashara na Uwekezaji Bi. Mwajabu Nyamkomora, amesema uwekezaji uliofanywa na Serikali katika miundombinu, utasaidia kuhabarisha umma juu ya maeneo yenye fursa za uwekezaji kwenye Utalii ambapo Mpango Mkakati huo pia, utafungua sura kwa wanadodoma na Watanzania kutambua fursa zilizopo.

Kadhalika, Bi. Nyamkomora aliwapitisha Wajumbe kwenye maudhui yaliyomo ndani ya Kitabu hicho kilichoshiba taarifa za vivutio adhimu vya Utalii vinavyopatikana katika Halmashauri za Mkao wa Dodoma ambavyo vingi havijulikani kama vinapatikana Mkoani hapa.

Kitabu cha Mpango Mkakati wa kukuza na kutangaza Utalii Mkoa wa Dodoma kinatarajiwa kuufungua Mkoa huu kwa vivutio vya Utalii ambapo Sekta hiyo ni moja ya vipaumbele vya Serikali ya Mkoa katika kuinua uchumi wa Wananchi na wa Mkoa kwa ujumla, kitabu hicho kinatarajiwa kuzinduliwa rasmi kwenye hafla itakayofanyika Agosti 04, 2025 katika Ukumbi wa Mabele Jijini hapa.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • SERIKALI IMEJIPANGA KUHAKIKISHA WAFANYABIASHARA WANAKUWA NA MAZINGIRA RAFIKI

    July 14, 2025
  • MZUMBE MBIONI KUANZA KAMPASI DODOMA

    July 14, 2025
  • AMANI YA NCHI YATAJWA KUWA AJENDA YA VIONGOZI WA SERIKALI NA WADINI

    July 13, 2025
  • DODOMA KUONDOKANA NA UKAME KUTOKANA NA UWEKEZAJI KATIKA MIRADI MIKUBWA YA UMWAGILIAJI

    July 13, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.