• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mkuu wa Mkoa Amshukuru Mhe. Rais Kwa Miradi Mikubwa na ya Kimkakati Mkoani Dodoma

Imetumwa : September 9th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameahidi kuwa, Serikali itafuatilia na kufanya uchunguzi wa kina wa malalamiko ya kuwepo kwa vitendo vya Rushwa vinavyofanywa na Maafisa Wanaohusika kutoa ajira kwa vijana kwenye makampuni ya ujenzi yanayojenga miradi ya Miundombinu mbalimbali inayojengwa Mkoani Dodoma Makao Makuu ya nchi.

Mhe. Senyamule ameyasema hayo mapema leo wakati alipofanya ziara ya kutembelea mradi wa ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato unaojengwa Jijini Dodoma na Mkandarasi aliyeshinda zabuni ya ujenzi wa mradi huo Kampuni ya SINO HYDRO kutoka nchini China ambapo alikutana na Kundi la vijana wanaoomba kazi kwenye Kampuni hiyo ambao walimlalamikia kuwa kazi katika Kampuni hiyo zinatolewa kwa vijana kutoa Rushwa kwa Maafisa Wanaohusika na kutoa ajira katika Kampuni hiyo.

Mhe Senyamule amesema kuwa Serikali kupitia vyombo vyake ikijiridhisha kuwepo kwa vitendo vya Rushwa Kama ilivyolalamikiwa na vijana hao, basi wote watakaokuwa wamehusika katika vitendo hivyo wataachukuliwa hatua kali za kisheria bila kumuacha mtu hata mmoja aliyehusika.

Mhe. Senyamule amemshukuru Mhe Rais Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo Serikali yake inajenga miradi MIKUBWA na ya KIMKAKATI Mkoani Dodoma Makao Makuu ya nchi na Mikoa mingine kwa Maendeleo ya nchi yetu na kuwa kupitia miradi hiyo pia Serikali inatakaa vijana wanufaike kwa kupata ajira kwenye miradi hiyo bila urasimu wa Rushwa au aina yoyote ya vikwazo.

Amesema kuwa mradi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Msalato kwa kuanzia umetoa ajira kwa vijana zaidi ya 300, mradi wa ujenzi wa Mji wa Serikali Mtumba umeajiri zaidi ya Vijana 8000, mradi wa Reli ya kisasa ya SGR kipande cha Dodoma umeajiri zaidi ya Vijana 6000, mradi wa Barabara ya Mzunguko wa Nje ya Jiji la Dodoma umeajiri zaidi ya Vijana 800 na pia ipo miradi mingine mingi Mkoani Dodoma Makao Makuu ya nchi.

Amewataka vijana waliopata ajira katika miradi hiyo Mkoani Dodoma kufanya kazi kwa bidii, uadilifu, nidhamu na pia wawe Walinzi wa Miradi hiyo na kutoruhusu tabia za wizi wa Vifaa vya Ujenzi, Mafuta ya mitambo na mashine mbalimbali. Amewataka kutumia miradi hiyo mikubwa Kama sehemu ya darasa Kwao kwamba wakitoka kwenye miradi hiyo wahakikishe wamepata ujuzi wa kutosha wa ujenzi kwenye fani mbalimbali.

Kwa upande wa Vijana waliokuwa wanatafuta ajira kwenye Kampuni hiyo ya SINO HYDRO katika mradi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Msalato, wamemlalamikia Mkuu wa Mkoa kuwa wamekuwa wakisubiria ajira hizo kwa miezi kadhaa bila kuzipata na kuongeza kuwa Ajira kwenye Kampuni hiyo zinapatikana baada ya mtu kutoa Rushwa kwa Maafisa wanaoajiri Jambo lililowakosesha ajira hizo na matokeo yake watu kutoka Maeneo ya mbali wenye uwezo wa kutoa Rushwa ndio wanakuja wanapewa ajira hizo.

SHIJA RICHARD ambae ni dereva wa magari makubwa amelalamikia kwa Mkuu wa Mkoa kuwa katika Kampuni hiyo ya SINO HYDRO ukitaka upate gari au mashine ya kuiendesha lazima uwe na laki moja ya kuwapa Maafisa Utumishi waajiri vinginevyo haupati kazi.

"Mimi nipo hapahapa zaidi ya miezi minne nasubiria kupata kazi baada ya kuwasilisha maombi na bado Sina kazi na kazi ninao uwezo wa kuzifanya lakini hatupewi, baadae unashangaa wanakuja watu wa mbali wanapewa kazi hizo baaaada ya kuhonga" aliongeza kijana Shija Richard.

Nae Khalid Fidelisi ambae ni Dereva wa Magari makubwa na mtambo wa kuchanganya Zege amemlalamikia Mhe. Senyamule kuwa amekuwepo hapo kwenye eneo la mradi kwa takribani miezi 3 bila kupata kazi.

"Sijapata kazi kwa muda wote huo, wanakuja watu wa nje wanapata kazi sisi tunasubiria nje hapa ya geti kupata mradi. niliwapa CV na barua ya maombi" aliongeza Khalid.

Kwa upande wake Afisa Rasilimaliwatu wa Kampuni hiyo ya SINO HYDRO Bw. Ndaki Maduhu amekanusha MADAI hayo na kusemaa kuwa siyo ya kweli, Jambo hilo halipo katika Kampuni yao. Amesema kuwa, mradi ndio umeanza kwa hatua za awali, bado kazi nyingi hazijaanza kufanyika ambazo zitachukua wafanyakazi wengi hivyo inalazimika kuchukua wachache kulingana na mahitaji ya mradi Jambo linalowafanya vijana wengi waendelee kusubiri.

Amesema kuwa utaratibu wa kutoa ajira kwenye Kampuni hiyo unawataka vijana kuwasilisha maombi yao ya barua yakiambatana na Wasifu wa muombaji (CV) ambavyo vinafanyiwa mapitio na uchambuzi na baadae waombaji wanafanyiwa majaribio ya vitendo kwa kupewa magari, mashine na mitambo waendeshe ili kubaini uwezo wao.

Nae Mhandisi Colman kutoka Wakala wa Barabara Tanzania - TANROADS Mkoa wa Dodoma amesema kuwa mradi wa Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Msalato umeanza Aprili 2022 unatakiwa kukamilika kabla au ifikapo Aprili 2025.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MMUYA AHIMIZA UDHIBITI VIFO VYA MAMA NA MTOTO

    May 26, 2025
  • UHAKIKI ANUANI ZA MAKAZI KUANZA MEI 28 DODOMA

    May 26, 2025
  • WAWEKEZAJI WA VIWANDA KUTOKA DUBAI WABISHA HODI DODOMA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI KUTOKA TUME YA MADINI WAMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.