• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

MUHIMILI WA MAHAKAMA WAKUTANA DODOMA, WASISITIZA UADILIFU

Imetumwa : October 10th, 2022

Muhimili wa Mahakama ukiongozwa na Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Juma umekutana kwenye Mkutano wa Tume ya Utumishi wa Mahakama na Wajumbe wa kamati za maadili za Mkoa wa Dodoma ambao umefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Mkutano huo umehusisha wajumbe wa Tume ya Utumishi wa mahakama wakiongozwa na Jaji Mkuu, ambaye ndiye Mwenyekiti wa Tume, Mwanasheria Mkiuu wa Serikali, Jaji mmoja wa mahakama ya Rufani, Jaji Kiongozi pamoja na wajumbe wawili ambao huteuliwa na Rais,kikao hicho pia kimehudhuriwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule,katibu Tawala wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Fatuma Mganga pamoja na wakuu wa Wilaya Saba za Mkoa wa Dodoma.

Akifungua kikao hicho, Jaji Mkuu amesema kuwa katika jitihada za kuhakikisha watumishi wa Mahakama wanakua waadilifu kwenye utekelezaji wa majukumu yao, Tume imechukua hatua ya kuwafukuza kazi na kusimamisha baadhi ya watumishi waliobainika kwenda kinyume na maadili.

“Kuna baadhi ya watumishi wa Mahakama wamefukuzwa kazi na wengine kusimamishwa kwa kukiuka maadili ya taaluma yao na kushindwa kusimamia haki za wananchi, hii itasaidia kuongeza uadilifu kwa watumishi wa Mahakama”  Amesema Prof. Juma.

Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Senyamule, ameishukuru Serikali kwa kuamua kujenga jengo la Mahakama Kuu Mkoani  Dodoma.

“Nimepata nafasi ya kulitembelea jengo linalojengwa kwa ajili ya Mahakama kuu, kwa kweli ni kubwa, zuri na lenye ubora. Huu ni utashi wa hali ya juu wa Serikali yetu kwani limetumia kiasi cha Shilingi Bilioni 129” Amesema

Kadhalika Mhe. Senyamule ameongeza kuwa Serikali ya Mkoa haina hiyari katika kushirikiana na Mahakama kwani ni wajibu wake ili Mtanzania aweze kupata stahili zake pia amesema uwepo wa kamati hizi unawakutanisha na wadau muhimu katika kuboresha maadili ya Mahakimu.

Naye Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Bw. Ilvin Mgeta, amefafanua muundo wa tume na kamati zake pamoja na majukumu yake ambapo miongoni mwa majukumu yake ni kumshauri Rais, kuchambua malalamiko dhidi ya Jaji wa Rufani, Jaji Kiongozi au Afisa yeyote wa Mahakama.

“ Majukumu mengine ni pamoja na kuchukua hatua za kiutawala dhidi ya Jaji wa Rufani, Jaji Kiongozi au Jaji, mbali na hatua zilizoainishwa katika Katiba, kuteua, kupandisha cheo na kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya watumishi wote isipokua kwa wale ambao sio mamlaka ya uteuzi wa Tume pamoja na kupandisha cheo au kuchukua hatua za kinidhamu dhidi ya mtumishi yeyote ambaye si afisa wa Mahakama kama ilivyoainishwa katika sheria” Bw. Mgeta

Tume ya Utumishi wa Mahakama imeanzishwa kwa mujibu wa ibara ya 112(1) ya Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ikisomwa pamoja na sheria ya uendeshaji wa Mahakama Na. 4 ya mwaka 2011. Kwa mujibu wa Kifungu Na. 15(1) cha sheria, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ndiye Katibu wa Tume na Mtekelezaji wa maamuzi ya Tume.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MMUYA AHIMIZA UDHIBITI VIFO VYA MAMA NA MTOTO

    May 26, 2025
  • UHAKIKI ANUANI ZA MAKAZI KUANZA MEI 28 DODOMA

    May 26, 2025
  • WAWEKEZAJI WA VIWANDA KUTOKA DUBAI WABISHA HODI DODOMA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI KUTOKA TUME YA MADINI WAMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.