• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC DKT. MAHENGE AZIAGIZA HALMASHAURI ZA WILAYA MKOANI DODOMA KUWATEMBELEA WAKULIMA KWENYE KATA NA VIJIJI KUWAPA HUDUMA ZA UGANI NA KUPATA TAARIFA HALISI ZA UZALISHAJI CHAKULA

Imetumwa : January 29th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge Januari 29, 2020 amefanya ziara ya kukagua shughuli za kilimo na uzalishaji chakula na mazao ya biashara kwenye Wilaya ya Mpwapwa na kutoa maagizo kwa Halmashauri za Wilaya Mkoani Dodoma kupitia idara zake za kilimo kuunda kamati na kuweka utaratibu wa kutembelea kata zote na vijiji kukagua namna wananchi wanavyoendesha shughuli za kilimo msimu huu wa mvua ili kuwasaidia utaalamu wa kilimo na pia kukusanya takwimu halisia za uzalishaji wa chakula na mazao ya biashara kutoka mashambani.

Dkt. Mahenge pia aliiagiza Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa kuandaa andiko kwa ajili ya ujenzi wa Skimu za kilimo cha umwagiliaji za Lumuma na Msagali ambazo Halmashauri hiyo imezitambua kama miradi ya kimkakati kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya chakula na Biashara kwa ajili ya kulisha Mkoa wa Dodoma Makao Makuu ya nchi. Dkt. Mahenge ameitaka Halmashauri ya Mpwapwa kuandaa andiko hilo ili Mkoa usaidie katika kufanya mawasiliano na Serikali kwa lengo la kupata fedha za kutekeleza miradi hiyo. 

Dkt. Mahenge ametumia ziara hiyo kuwataka wananchi kutumia mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani Dodoma kujizalishia chakula cha kutosha na mazao ya kibiashara.

“Sitarajii mwaka huu mwananchi alalamike njaa wakati mvua zinanyesha za kutosha maeneo yote kwa kiwango kinachotuwezesha kuzalisha chakula cha kutosha, Halmashauri za Wilaya kupitia idara za kilimo ziunde kamati za kupita kukagua shughuli za kilimo mashambani kwenye Kata na Vijiji ili kuweza kuwasaidia wakulima huduma za utaalamu na pia kupata takwimu halisi na sahihi za uzalishaji mazao ya chakula na biashara” alikazia Dkt. Mahange. 

Dkt. Mahenge alibainisha kuwa ujenzi wa miradi ya skimu za kilimo cha umwagiliaji kwa kujenga mabwawa makubwa ya kuvuna maji ya mvua zitasaidia wananchi waendeshe shughuli za kilimo na uzalishaji chakula na mazao ya biashara kwa kipindi cha mwaka mzima na pia utapunguza athari za mafuriko yanayosababishwa na mvua zinazoendelea kunyesha Mkoani Dodoma.

Kwa upande wake Afisa Kilimo wa Wilaya ya Mpwapwa 

amesema kuwa malengo ya uzalishaji kilimo kwa msimu wa mwaka 2019/2020 jumla ya kaya 81,392 zinashiriki katika shughuli za kilimo, ambapo kwa mazao ya chakula jumla ya Hekta 93,209 zinalimwa na kuwa zitazalisha Tani 137,572. Aidha, amesema kwa mazao ya biashara jumla ya Hekta 43,568 zinalimwa na kuwa zitazalisha Tani 57,684.

Amesema kwa upande wa mazao ya bustani jumla ya Hekta 653 zinalimwa na matarajio yaliyopo watazalisha Tani 9,407 ambapo mazao ya chakula ni pamoja na mtama,mahindi, uwele, mpunga, mhogo, maharage na viazi. Kwa upande wa mazao ya Biashara ni pamoja na Karanga, Alizeti, Ufuta na Korosho. Aliongeza kuwa mazao ya bustani wanayolima haswa skimu ya Lumuma ni pamoja na Vitunguu na Nyanya.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.