• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC DKT. MAHENGE AZITAKA HALMASHAURI ZOTE MKOANI DODOMA KUTENGA FEDHA ZA KUTEKELEZA AFUA ZA LISHE KUPAMBANA NA UTAPIAMLO

Imetumwa : February 7th, 2020

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt Binilith Mahenge amezitaka Halmashauri za mkoa wa Dodoma kutenga fedha ili kukabiliana na utapiamlo na lishe duni kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano kutokana na tathmini kuonyesha kuwa watoto 9,767 wanakabiliwa na suala la lishe duni.

Dk Binilith Mahenge ametoa kauli hiyo leo jijini Dodoma wakati akifungua kikao cha kutathmini utekelezaji wa mkakati wa lishe kwenye mkoa wa Dodoma kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Disemba mwaka 2019, kikao kilichohudhuriwa na viongozi wa Wilaya na Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma, wataalamu wa masuala ya lishe kutoka Halmashauri zote za Dodoma na wadau mbalimbali wanaounga mkono programu za lishe kwenye Mkoa wa Dodoma.

Dk.Mahenge amesema kuwa kila halmashauri imetenga kwenye bajeti kiasi cha fedha kwa ajili ya kukabiliana na suala la lishe duni kwa akina mama wajawazito na watoto walio chini ya miaka mitano lakini utekelezaji wake umekuwa wa kusuasua.

“Kila Halmashauri inatakiwa kutenga sh 1,000 kwa kila mtoto kwa ajili ya kukabiliana na utapiamlo kwa watoto walio chini ya miaka mitano lakini cha kusikitisha kuna baadhi ya Halimashauri hazitekelezi agizo hili hali inayoturudisha nyuma kwenye suala zima la mapambano dhidi ya utapiamlo,” amesema Dk.Mahenge

Aidha ametoa agizo kwa wale wote wanaohusika na utoaji wa mafungu ya fedha za kukabiliana na tatizo la lishe duni kwa kila Halmashauri kufanya hivyo ili tukikutana tena mwezi wa sita mwaka huu tuwe tumefanya vizuri zaidi.

Awali Afisa lishe wa mkoa wa Dodoma, Heriet Carin amesema kuwa jumla ya Sh 543.88 milion zilitengwa kwa ajili ya kukabiliana na utapiamlo kwa watoto chini ya miaka mitano kwa mwaka 2019/20 lakini fedha zilizotolewa ni Sh 120.74 milioni ambazo ni sawa na asilimia 48 ya fedha yote iliyotengwa.

Bi.Carin amesema kuwa tathmini iliyofanywa na Mkoa ili kugundua watoto wenye utapiamlo mkali, udumavu na uzito mdogo uligundua kuwa kulikuwa na watoto 9,767 waliokuwa wanakabiliwa na suala la lishe duni mkoani hapa.

”Hivyo Halmashauri zote natazitaka zitoe kipaumbele katika masuala ya lishe kwenye bajeti zao ili kukomesha utapiamlo na kutengeneza kizazi chenye afya njema kwa maendeleo ya Taifa”amesema Bi.Carin

Mkuu wa Mkoa Dkt. Mahenge alitumia kikao hiko cha tathimini ya masuala ya Lishe pia kuzindua kitabu cha Mkakati wa lishe wa Mkoa wa Dodoma na kuwagawia makundi yote muhimu yanayoshirikiana kuratibu masuala ya lishe Mkoani Dodoma kuanzia Sekretarieti ya Mkoa, Viongozi wa Wilaya zote za Mkoa wa Dodoma na Halmashauri zote kwenye Mkoa wa Dodoma na wadau wa Lishe.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.