• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC MTAKA AKABIDHIWA RASMI OFISI, ATAJA VIPAUMBELE VYAKE VIKIONGOZWA NA ELIMU

Imetumwa : May 21st, 2021

MAKABIDHIANO YA OFISI: Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka akielezea vipaumbele vyake kwenye Mkoa wa Dodoma wakati wa hafla fupi ya Makabidhiano ya Ofisi kati yake na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye kwa sasa amehamishiwa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge iliyofanyika Mei 21, 2021.

MAKABIDHIANO YA OFISI: Dkt. Binilith Mahenge (kulia) aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma ambaye kwa sasa amehamishiwa Mkoa wa Singida, akitoa salamu za shukrani kwa viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Dodoma na Taasisi zake wakati wa hafla ya kumkabidhi ofisi Mkuu mpya wa Mkoa wa Dodoma  Mhe. Anthony Mtaka, hafla hiyo imefanyika Mei 21, 2021.

Picha za pamoja mara baada ya hafla ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka kukabidhiwa rasmi ofisi na mtangulizi wake Dkt. Binilith Mahenge aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na sasa kahamishiwa Mkoani Singida.


..................................................................................................................................................................................................................................................

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony John Mtaka, leo Mei 21, 2021 amekabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa huo  Dkt. Binilith Mahenge ambaye kwa sasa  amehamishiwa Mkoani Singida; Mhe. Mtaka ametumia hafla hiyo fupi ya makabidhiano ya ofisi kuelezea vipaumbele vyake katika Mkoa wa Dodoma, huku akitaji elimu kuwa kipaumbele cha kwanza kwa kipindi chote atakachoongoza Mkoa wa Dodoma.

Mhe. Mtaka amesema kuwa elimu kwake ni kipaumbele kikubwa sana na kinaanzia kwenye ngazi ya familia na kusisitiza kuwa, Watoto kwenye Mkoa wa Dodoma ni lazima wasome aidha wanapenda au hawapendi lengo likiwa kuandaa kizazi kipya cha Makao Makuu ya nchi chenye elimu inayoendana na hadhi ya Mkoa wa Dodoma.

Mhe. Mtaka amestaajabu kiwango cha chini cha elimu na ufaulu kwenye Mkoa wa Dodoma ambao ndio Makao Makuu ya nchi ukilinganisha na Mkoa kama wa Simiyu ambapo alishangaa shule ya kwanza kwa ufaulu Dodoma inashika nafasi ya 103 Kitaifa wakati shule ya kwanza kwa ufaulu Mkoani Simiyu inashika nafasi ishirini bora Kitaifa.

“Wakurugenzi na Maafisa elimu katika Mkoa wa Dodoma tujiandae katika kutekeleza azma hii huku tukishirikiana na Wazazi na Walimu kuhakikisha tunasomesha watoto wetu, tunawajengea uwezo  wa kupenda elimu “ alifafanua Mhe. Mtaka huku akisema Mkoa kama Dar es salaam una chuo kikuu kikubwa cha Dar es salaam ambacho kimechangia Mkoa huo kuwa na uchumi mkubwa na hata nchi ya Afrika Kusini ina vyuo vikuu vikubwa na hivyo kusaidia nchi hiyo kuwa na uchumi mkubwa akitaka pia Mkoa wa Dodoma kuweka mkazo katika elimu kwa kuwa itasaidia kukuza maendeleo na uchumi wa Mkoa.

Katika hatua nyingine, Mhe. Mtaka ametoa wito kwa Mkuu wa  Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge kushirikiana pamoja ili kuiwezesha Mikoa hii miwili ya Kanda ya Kati kujikita katika kilimo bora na cha kibiashara cha zao la Alizeti ili kuweza kuzalisha kiasi kikubwa cha mafuta ya chakula na kuondoa utegemezi wa nchi yetu kuagiza karibu tani laki tano za mafuta ya chakula ambapo wakulima wa Singida na Dodoma wanaweza kuzalisha Alizeti ya kutosha kuzalisha kiasi hiko cha mafuta jambo ambalo litakuza sekta ya viwanda vya kuongeza thamani ya mazao yanayozalishwa.

Mhe. Mtaka pia ameahidi kushirikiana kwa karibu na sekta binafsi katika Mkoa wa Dodoma kwa kuwa anatambua kuwa sekta Binafsi ni kiungo muhimu kabisa katika kukuza uchumi wa Mkoa wa Dodoma na kwamba sekta binafsi inazalisha na kukuza ajira, biashara na uwekezaji; vitu vinavyochangia kukuza pato la Mkoa na kuongeza mchango katika pato la Taifa. Kutokana na Dodoma kuwa Makao Makuu ya nchi, amewataka viongozi na watendaji wote kuwa na kauli nzuri kwa wawekezaji wanapokuja kutaka kuwekeza Dodoma ili kusisimua uchumi wa Mkoa wa Dodoma.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge, ametumia hafla hiyo ya kumkabidhi ofisi Mhe. Mtaka, kuwashukuru Viongozi na Watendaji wote wa Mkoa wa Dodoma na Taasisi zake kwa ushirikiano mkubwa waliompatia wakati akiwa Mkuu wa Mkoa huo; ushirikiano uliowezesha kutekeleza na kufanikisha mambo mengi ya msingi kwenye Mkoa wa Dodoma na kuwaomba Viongozi na Watendaji  hao kuongeza zaidi ushirikiano kwa Mkuu wa Mkoa wa sasa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

    May 03, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.