• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC MTAKA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS NA WAZIRI MKUU MSTAAFU MZEE JOHN SAMWEL MALECELA, AMSHIRIKISHA VIPAUMBELE VYAKE KATIKA MKOA WA DODOMA

Imetumwa : June 9th, 2021

HABARI PICHA KATIKA PICHA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka akimsikiliza Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Samwel Malecela


Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Samwel Malecela akimuonesha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka kumbukumbu mbalimbali zilizohifadhiwa kwa njia ya picha katika Makazi yake yaliyopo eneo la Uzunguni Jijini Dodoma


Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Samwel Malecela akimsindikiza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka mara baada ya kumaliza mazungumzo yao yaliyofanyika nyumbani kwa Mzee Malecela eneo la Uzunguni Jijini Dodoma

.......................................................................................................................................................................................................................................................


RC MTAKA AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MAKAMU WA KWANZA WA RAIS NA WAZIRI MKUU MSTAAFU MZEE JOHN SAMWEL MALECELA, AMSHIRIKISHA VIPAUMBELE VYAKE KATIKA MKOA WA DODOMA

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony Mtaka, katikati ya wiki amekutana na kufanya mazungumzo na Makamu wa Kwanza wa Rais na Waziri Mkuu Mstaafu Mzee John Samweli Malecela ambapo ametumia nafasi hiyo kumshirikisha Mzee Malecela vipaumbele vyake katika Mkoa wa Dodoma na kupokea ushauri wa kiongozi na mwanasiasa huyo Mkongwe hapa nchini.


Mhe. Mtaka aliyemtembelea Mzee Malecela nyumbani kwake eneo la uzunguni hapa Jijini Dodoma, amemwelezea Mzee Malecela kuwa kipaumbele chake cha kwanza hapa Mkoani Dodoma ni Elimu na kazi iliyombele ni kunyanyua kiwango cha Elimu na Ufaulu katika Mkoa wa Dodoma. Katika kuleta mabadiliko hayo ya Elimu, Mhe. Mtaka amesema atashirikiana na viongozi wazawa wa Mkoa wa Dodoma, wadau wote wenye jukumu la kusimamia elimu kuanzia ngazi ya Mkoa, Wilaya na Mamlaka za Serikali za Mitaa hadi Ngazi za Msingi hali kadhalika sekta binafsi.


Akitaja kipaumbele kingine Mhe. Mtaka amesema atageukia sekta ya kilimo kwa kuzifanya Wilaya za Pembezoni za Mkoa wa Dodoma (Wilaya zinazozunguka Wilaya ya Dodoma) kuwa Kanda Maalum za Kilimo na kukifanya Kilimo cha Mkoa wa Dodoma kuwa cha kibiashara huku mkazo akiuweka kwenye zao la Zabibu kama alama ya Mkoa wa Dodoma, Alizeti na mazao mengine ya kuzalisha mafuta ya chakula. Amesema kilimo kitasaidia kukuza uchumi wa Wilaya za Mkoa wa Dodoma na Mkoa kwa ujumla.


Mhe. Mtaka amemwelezea Mzee Malecela kuwa mahitaji makubwa ya mafuta ya chakula yanayoilazimu nchi yetu kuagiza mafuta nje ya nchi, ni fursa kubwa ya kiuchumi kwa Mkoa wa Dodoma ambao mazao yanayotumika kuzalisha mafuta kama Alizeti, Karanga na Ufuta yanastawi vizuri katika Mkoa wa Dodoma.


Katika Mazingira, Mhe. Mtaka amesema ataendesha kampeni ya Mkoa ya Upandaji na ustawishaji miti katika Mkoa Mzima wa Dodoma itakayo shirikisha Wadau wa ngazi mbalimbali kuanzia Mkoa, Wilaya, Tarafa, Kata, Vijiji, Vitongoji na ngazi za kaya. Mhe. Mtaka amemtaja Mzee Malecela kama mfano wa kuigwa wa wana mazingira ambao walifanikisha kupanda miti mingi kwenye maeneo waliyokuwa wanayaongoza.


Nae Mzee Malecela ameshukuru kwa mazungumzo yaliyowezesha kubadilishana uzoefu na Mkuu wa Mkoa Mtaka, amesema Dodoma ina fursa kubwa ya kilimo cha mazao yanayokamuliwa kuzalisha mafuta ya chakula huku akizitaja Wilaya za Kongwa na Mpwapwa kama maeneo yenye hali ya hewa nzuri kwa uzalishaji wa Karanga tangu miaka ya zamani, ametaja maeneo ya Wilaya zingine za Dodoma yanafaa sana kwa kilimo cha Alizeti na Zabibu.


Amemtaka Mkuu wa Mkoa Mtaka kuweka mkazo pia kwenye sekta ya ufugaji kwa kutambua Mkoa wa Dodoma una idadi kubwa ya mifugo ambayo ni fursa nyingine ya kukuza uchumi wa Mkoa huku akibainisha kuwa pamoja na Mkoa kubahatika kuwa na kituo kikubwa cha utafiti wa mifugo cha Mpwapwa na shamba kubwa la Mifugo la Serikali lililopo Kongwa bado rasilimali hizo hazijasaidia kubadilisha jamii za Wafugaji wa Mkoa wa Dodoma kuweza kuwa na tija katika ufugaji wao huku wakiendelea kufuga mifugo kienyeji.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2020 January 15, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 SHULE ZA BWENI (WASICHANA NA WANAUME) . December 20, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KIWANDA CHA AINA YAKE KUJENGWA KONGWA

    March 17, 2023
  • WAFANYAKAZI WAASWA MSHIKAMANO MAHALA PA KAZI

    March 15, 2023
  • BILIONI 4.6 KUIBADILISHA RANCHI YA KONGWA

    March 15, 2023
  • SENYAMULE AWAKARIBISHA MABALOZI DODOMA

    March 15, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Mkoa akiongoza siku ya maombi jijini Dodoma
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.