• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE AFANYA UKAGUZI WA MIRADI YA HALMASHAURI YA DODOMA JIJI

Imetumwa : October 20th, 2022

RC SENYAMULE  AFANYA UKAGUZI WA MIRADI YA HALMASHAURI YA DODOMA JIJI

Ikiwa ni mwendelezo wa ziara za kutembelea miradi na kufanya vikao na watumishi pamoja na wananchi wa Halmashauri za Mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Mkoa Mhe. Rosemary Senyamule amefanya ziara ya ukaguzi wa miradi inayotekelezwa na Halmashauri ya Dodoma Jiji.

Katika ziara hii Mkuu wa Mkoa ameambatana na Katibu Tawala Mkoa Dkt. Fatuma Mganga, Kamati kuu ya Ulinzi na Usalama Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Jiji Mhe. Jabir Shekimweri pamoja na wakuu wa Taasisi pamoja na Idara mbalimbali za Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Mkoa. Ziara hiyo imeanzia kwenye ukaguzi wa miradi ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa kituo cha afya cha Nkuhungu.

Ujenzi wa Kituo hiki cha afya unafanbyika katika eneo lenye  ukubwa wa SQM 14,000, mpaka kukamilika kwake mradi huu unatarajiwa kugharimu kiasi cha Tsh Milioni 210 ambazo ni fedha kutoka kwenye mfuko wa mapato ya ndani ya Halmashauri. Aidha kituo hicho kitasaidia kupunguza changamoto ya wakazi wa eneo hilo kufuata huduma za afya umbali mrefu. Ujenzi unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Desemba mwaka huu.

Baada ya Nkuhungu, Mkuu wa Mkoa na msafara wake wametembelea mradi wa ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa pamoja na mabweni mawili katika shule ya sekondari ya wavulana ya Bihawana  ambapo ujenzi huo unagharimu shilingi Milioni 240 na umeanza kutekelezwa toka tarehe 11 Julai 2022 na unatarajiwa kukamilika tarehe 30 Novemba 2022.

Mradi mwingine uliotembelewa na msafara wa Mkuu wa Mkoa ni ujenzi wa shule ya msingi Msangalale ambayo ni ya Serikali itakayotumia mtaala wa Kiingereza inayojengwa katika eneo la Mapinduzi East, Msangalale - Dodoma Makulu. Mradi wa ujenzi unagharimu Tsh Milioni 750 zilizotoka kwenye Taasisi ya Elimu nchini (TEA). Mradi wa shule hii ya kisasa unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba, 2022 na inatarajiwa kuanza kufundisha Januari 2023.

Shule ya sekondari Mtemi Chiloloma inayopatikana katika Kata ya Hombolo Makulu, ndio mradi wa mwisho kutembelewa na msafara huu ambapo shule hiyo mpya inatarajiwa kuwa na madarasa manne (4), mabweni matatu (3), matundu 20 ya vyoo na majengo mengine. Mradi ulianza kutekelezwa Januari 2022 na unatarajiwa kukamilika Mwezi Novemba 2022. Tayari shule imeanza Oktoba 10 mwaka huu kwa kupokea wanafunzi 142 wa kidato cha kwanza.

Mhe. Senyamule ametoa pongezi kwa Halmashauri ya Jiji kwa kuanzisha miradi hiyo ambayo itasaidia kusukuma gurudumu la maendeleo kwa nchi yetu licha ya kuwataka kuikamilisha kwa wakati kama walivyoahidi ili kuleta tija licha ya changamoto kadhaa zilizojitokeza katika utekelezaji wake, aidha amewataka kuhakikisha kuwa wanakabiliana na changamoto huku Serikali ya Mkoa ikitoa ushirikiano wa karibu kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.