• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE AIPA KONGOLE FOUNTAIN GATE ACADEMY

Imetumwa : September 1st, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Rosemary Senyamule ameipongeza Taasisi ya Fountain Gate Academy kwa kuamua kuwezesha katika elimu na kukuza michezo kwa vijana kupitia academy ya Fountain Gate Dodoma.

 Akizungumza leo na waandishi wa habari leo Septemba 1,2023 Jijini Dar es Salaam katika hafla fupi ya kumuaga binti Mary Siyame anayekwenda nchini Hispania kwenye masomo na Mafunzo ya mpira wa miguu katika Academy ya Laliga (Ligi Kuu ya Soka ya Hispania), Mhe. Senyamule amesema kazi ambayo inafanywa na taasisi hiyo kutoa elimu na kukuza vipaji vya michezo inaunga mkono jitihada za Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ambapo ameweka nguvu kubwa katika sekta ya michezo, burudani, sanaa na fani mbalimbali ambayo imeweza kuwapa ajira na kuwanufaisha wanamichezo na wasanii mbalimbali.

 Amesema Kipaji na michezo ni fursa kiuchumi na kuingiza fedha nyingi ” mfano hai tunaona namna wanamichezo wengi leo walivyo matajiri hapa kwetu na nchi mbalimbali”.

 Aidha Mhe.Senyamule amempongeza binti Marry kwa hatua ambayo ameifikia na juhudi ambazo amezionesha na kupata fursa ya kupelekwa nje ya nchi kwaajili ya kuendeleza kipaji chake.

 “Nenda ukaongeze elimu ya michezo huko nchini Hispania ili ufike mbali na kupata elimu bora na upate timu kubwa kuzichezea Hispania na Duniani katika mpira wa kulipwa”. Ameeleza Mhe.Senyamule.

 Pamoja na hayo amemtaka akawe balozi mzuri wa Taifa la Tanzania na kuiletea sifa ma heshima na kuweza kufungua milango kwa watoto wengine zaidi wa kitanzania kufika mbali. Hata hivyo amewataka wazazi na walezi kuzingatia kuwa na malezi bora yenye misingi ya maadili ya Kiitanzania ili kupata vijana waadilifu watakao lisaidia Taifa katika maeneo mbalimbali.

Nae Afisa mahusiano ya kimataifa – Fountain Gate Bw.Dennis Joel amesema binti Mary amekuwa mzuri kwenye masomo yake, kwenye nidhamu na ndo maana amepata fursa ya kwenda nchini Hispania.

“Sisi kama Fountain Gate Academy, kama mtoto anakipaji lakini hana nidhamu, huyo hatokuwa pamoja na sisi, na kuna ambao tumeshawatoa kwasababu hizi kwa maana anakipaji kikubwa lakini hana nidhamu”. Amesema Bw.Joel.

 Amesema wamekuwa wakiwapeleka wanamichezo wenye vipaji vya mpira wa miguu nchini Hispania ambapo wanafanyiwa majaribio kwa timu kama Barcelona Fc, hivyo muda wowote wakihitajika wanaweza kuitwa. Pamoja na hayo amesema wanajivunia kwa kupeleka mwanafunzi ambaye ataenda kuwawakilisha vyema hasa kutokana na malezi bora aliyoyapata kupitia taaisisi hiyo.

 

Kwa upande wake Mary Siyame ambaye amepata fursa hiyo amesema anaenda akuiwakilisha vizuri Mkoa wa Dodoma pamoja na nchi yake kwa ujumla hasa kwa kuhakikisha anafanya vizuri kwenye masomo yake pamoja na michezo kupitia kipaji chake cha mpira wa miguu.

 

Amesema matarajio yake ni kuwa mchezaji mkubwa ambaye anaweza kusimama na kila mtu akaweza kumfahamu Duniani kupitia kipaji chake kwenye mpira wa miguu.

 “Kwa kuwa Rais wetu Dkt.Samia Suluhu Hassani amekuwa mstari wa mbele kwa kuunga mkono juhudi za wanamichezo wanawake nchini, namuhakikishia ninakwenda kufanya vizuri”. Amesema binti Mary.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.