• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE ATEMBELEA MAJERUHI WA AJALI LA LORI NA BASI

Imetumwa : September 18th, 2025

_ awataka madereva kuzingatia sheria za usalama barabarani

Na Sofia Remmi,

Habari-DodomaRs.

Mkuu  wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule leo tarehe 18 Septemba 2025 amewatembele majeruhi wa ajali ya lori na basi iliyosababisha vifo vya watu 09 na majeruhi 16 baada ya basi walilokuwa wakisafiria kugongana na lori eneo la Kambi ya Nyasa wilaya ya Chemba mkoani Dodoma.

Akizungumza baada ya kutembelea majeruhi waliolazwa katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Dodoma.Mhe. Senyamule amesema,

Majeruhi wengine walipelekwa hospitali ya wilaya ya Chemba ambapo majeruhi wanne walifariki njiani na wengine walifariki wakiwa hospitali hapo na kusababisha vifo kufikia tisa 09 na majeruhi 16,majeruhi tisa walihamishiwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya matibabu zaidi.

‘Tumesikitika kupoteza Watanzania wenzetu kutokana na ajali hiyo mbaya, tunashukuru waliokuwa mstari wa mbele kuokoa waliopata ajali na hata kusafirisha salama majeruhi wengine kufikishwa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Dodoma

Eneo lililotokea ajali ni eneo ambalo kama madereva wangekuwa makini,haikupaswa kutokea ajali kwa sababu,ni  barabara ya lami iliyonyooka, ni eneo salama ambalo kila moja ana uwezo wa kumuona mwenzake”Amesema Senyamule

Aidha,Mhe. Senyamule ametoa  wito kwa madereva kuzingatia sheria na kuwa makini.

'' ukiona usingizi unakuja simamisha gari ili upumzike, tungetamani maeneo yote watu wasafiri salama".Amesisitiza Mhe. Senyamule.

Kwa upande wake  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Gallus Hyera amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyotokea leo saa 1:40 asubuhi, ambapo basi linalojulikana kama Babu Trans lenye namba za usajili T.129 DVX aina ya Tata likitokea Kondoa kwenda Dodoma kugongana uso kwa uso na lori namba T.907 EJZ lililokuwa likitokea Dodoma kwenda Kondoa..

Amesema kuwa kati ya waliopoteza maisha ni dereva wa basi hilo pamoja na wanafunzi wanne, huku dereva wa lori akiwa miongoni mwa majeruhi.

Aliwataja wanafunzi waliofariki katika ajali hiyo kuwa ni  Caroline Joackim (13), Rukia Ally (14), Bashiru Hashim (13) na Nasra Mohamed (18).

Kamanda Hyera amesema kulingana na maelezo ya majeruhi na mashuhuda wa ajali hiyo, dereva wa lori alihama upande wake na kwenda upande wa kulia na kugongana uso kwa uso na basi.

Alitoa wito kwa madereva kuzingatia sheria za usalama wa barabarani kwani matukio ya uzembe yamekuwa yakigharimu maisha ya watu.

Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya Dodoma Ibenzi Ernest amesema kuwa wamepokea majeruhi tisa,

“Kuna baadhi wameumia kwenye miguu, mikono na baadhi wameumia kwenye kichwa,” Amesema.

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • HOSPITAL YA BENJAMIN MKAPA YAADHIMISHA MIAKA 10 YA MAFANIKIO

    October 13, 2025
  • SERIKALI INA DHAMIRA YA KILA MWANAMKE KUJIKOMBOA KIUCHUMI

    October 09, 2025
  • SACCOS NI FURSA KWA MAENDELEO YA KIUCHUMI YA WANAWAKE

    October 11, 2025
  • RC SENYAMULE AZUNGUMZA NA WAZEE WA MKOA WA DODOMA

    October 09, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.