• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RC SENYAMULE AZIELEKEZA TARURA NA TANROADS KUZIBUZ MIFEREJI YA MKONDO WA MAJI YA MVUA

Imetumwa : December 7th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule amezielekeza taasisi zinazohusika na ujenzi wa mifereji ya barabara ambazo ni Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kuhakikisha miferejii inazibuliwa na kutolewa uchafu wote ili kuruhusu maji kupita kwa haraka na kusaidia kupunguza athari zinazoweza kuletwa na mafuriko.

Maelekezo hayo yametolewa Disemba 6,2023 wakati wa ziara yake ya kikazi ya ukaguzi wa Miradi ya barabara za TARURA katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.

Mhe.Senyamule ametoa shime kwa wakandarasi kufanya kazi kwa kuzingatia ubora na wakati bila kujali hali ya hewa ya sasa kwani wakati wanasaini mikataba walikuwa wanajua watafanya kazi kwa nyakati zote za masika na kiangazi.

"Lakini tunajua muda huu tunaojenga ni muda wa mvua sasa tusiwe na sababu nyingi tangu wakandarasi wanasaini mkataba walijua kutakuwa na mvua kwa kujua wataanza lini na kumaliza lini ,hatutegemei mvua ikawa ndio sababu ya kutoa maelezo mengi ya kuchelewesha mradi .

"Lakini kikubwa nacho sisitiza ni uimara wa miradi Tunachotegemea watazingatia "amesema Senyamule

Katika Hatua nyingine, Mhe.Senyamule amesisitiza suala la mazingira katika kila barabara zinazojengwa sasa hivi kuhakikisha zinapandwa miti pembezoni ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa agizo la Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira la kutunza mazingira na kupendezesha barabara zenyewe.

"Nitoe wito kwa wakandarasi wote kabla hawajaondoka saiti lazima TARURA mjiridhishe kama miti imepandwa na kustawi pembezoni mwa mwabarabara " Amesisitiza Senyamule

Kadhalika,ameendelea kuhimiza kuchukua tahadhari za kujikinga na madhara yatakayoweza kujitokeza kutoka na mvua zinazo tarajiwa kunyesha kwa mujibu wa Mamlaka ya hewa nchini (TMA ) .

Katika ziara hiyo amefanikiwa kukagua barabara zenyewe urefu wa Kilometa 6.95 zinazojumuisha barabara ya Abeid Amani Karume 0.70km,Robina 0.65km, Malecela 1.80 Km, Ally Hassan mwinyi 1.00 Km, Rashidi Kawawa 1.90 Km na Mshikamano 0.9 Km pamoja na matengenezo ya barabara yenye jumla ya Km 1,396.73 ambapo Km 7.045 ni lami ,Km 550.065 ni tabaka la Changarawe na kiasi cha Km 839.62 ni tabaka la udongo sambamba na daraja lenye njia tatu za kupisha maji katika kijiji cha kihegea na daraja la mawe linalojengwa katika Kijiji cha Dabalo.



Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.