• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

‘SAMIA DAY’ YASHUHUDIA MAFANIKIO MAKUBWA KATA YA MAKOLE KIPINDI CHA MIAKA MINNE YA MHE. DKT SAMIA

Imetumwa : June 3rd, 2025

Na: Hellen M. Minja

       Habari - DODOMA RS

Mkoa wa Dodoma unashuhudia maendeleo makubwa na ya kasi kwa kipindi kifupi cha Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo Mkoa umeamua kuyaweka wazi kupitia maadhimisho ya siku ya Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ambayo ni maalum kwa kumpongeza na kumshukuru, yaliyopewa jina la 'Dodoma Samia day’ yaliyofanyika leo Juni 03, 2025 katika kata zote 209 zinazopatikana katika Halmashauri 8 za Mkoa wa Dodoma.

Mkuu wa Mkoa huu Mhe. Rosemary Senyamule, ameshiriki Maaadhimisho hayo kwenye Kata ya Makole Jijini Dodoma ambapo makundi mbalimbali yalihudhuria  kwa lengo la kuyasema mazuri hayo.

“Yupo mtu ambaye amefanya vitu vingi ambavyo katika historia ya Nchi yetu tangu Uhuru hatujawahi kushuhudia maendeleo ya muda mfupi kwa kasi kubwa kwa Mkoa wa Dodoma kama tulivyoshuhudia katika kipindi hiki. Tumesikia wakati wote watu wakisema, lazima vitu visemwe, tusipovisema sisi, wengine watasema kinyume chake.”

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri amesema katika Wilaya yake amepitia taarifa za miradi kwenye kila Kata jinsi ambavyo zimeguswa, ikiwemo miradi mikubwa ngazi ya Wilaya, miradi ya kimkakati na miradi ya wadau na kujiridhisha kwamba wametumia fedha zaidi ya shilingi Trilioni 1 kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo kwa Wilaya ya Dodoma pekee.

Hata hivyo, Diwani wa Kata ya Makole Mhe. Omary H. Omary amesema katika kipindi cha miaka mitano, Kata yake imepokea miradi mingi ikiwemo ujenzi wa Barabara za lami, madarasa ya muundo wa ghorofa katika shule ya msingi Makole, malipo ya fidia kiasi cha milioni 900 kwa wananchi waliokua wanasumbuliwa katika eneo la ‘D Center’ pamoja na ujenzi uliokamilika wa ofisi ya Machinga Mkoa.

Mmoja kati ya mashuhuda wa mambo yaliyofanywa na Serikali ya awamu ya sita ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kikundi cha ‘Wanawake na Samia’ Mkoa wa Dodoma Bi. Fatma Madidi, ameshuhudia mafanikio ya Serikali kwenye Kata ya Makole kwa upande wa nishati safi ya kupikia ya mkaa mbadala ambayo wao kama kikundi ni mawakala wa kuuza na kusambaza nishati hiyo inayozalishwa na Shirika la Madini STAMICO na mpaka sasa wameshauza tani 17 za mkaa huo.

Kata ya Makole ni miongoni mwa Kata 41 za Halmashauri ya Jiji la Dodoma inayokua kwa kasi kiuchumi, kisiasa na kijamii ikiwa na jumla ya wakazi 10,571. Kwa kipindi cha miaka minne, Kata hiyo imepokea jumla ya shilingi Bilioni 1.1 iliyotumika kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo ya Elimu, Maendeleo ya Jamii, Mikopo kwa wajasiriamali wa makundi maalumu pamoja na fedha za mpango wa kunusuru kaya Maskini (TASAF) zinazonufaisha Kaya 41.




#samiaday2025dodomatumetekeleza

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MRADI WA ‘KOFFI’ WATOA DOLA BILIONI 2.455 KUBORESHA HUDUMA ZA UZAZI NA MTOTO DODOMA

    August 21, 2025
  • WANANCHI NA WADAU WAASWA KUCHAGIZA UTALII - DODOMA

    August 21, 2025
  • WADAU WAASWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA JAMII DHIDI YA MAJANGA

    August 19, 2025
  • WAFANYABIASHARA WA MKOA WA DODOMA WATANGAZIWA FURSA ZA BIASHARA NCHINI INDONESIA

    August 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.