• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

"Sanaa na Utamaduni ni Ajira"-Rc Mtaka

Imetumwa : July 24th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Anthony  Mtaka ameeleza kuwa Sanaa, Utamaduni  na michezo ni fani zinazotoa ajira kwa vijana na kuchangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa nchi.

Mhe. Mtaka amesema hayo Julai 23, 2022 Chamwino Dodoma wakati akifungua Tamasha la 13 la Muziki wa Cigogo linaloazimishwa kila mwaka.

"Nawaomba wazazi na walezi kuwaruhusu  vijana wenu  kushiriki shughuli za  Sanaa , utamaduni na michezo ni mojawapo ya ajira ambazo  zinachangia  katika pato la taifa"amesema Mhe. Mtaka

Aidha Mhe. Mtaka ametoa wito  kwa waandaaji wa  tamasha la Cigogo kuliongezea thamani tamasha hilo ili lifikie kiwango cha kitaifa na kimataifa kama lilivyo  tamasha la Sauti za Busara la Zanzibar.

Vilevile Mhe. Mtaka ametumia nafasi hiyo,kumpongeza Mwanzilishi wa Tamasha hilo Dkt. Kedmon Mapana kwa kuaminiwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuteuliwa kuwa  Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) ambapo amemsihi kuendelea kukuza sanaa kwakua ni kazi ambayo anaijua vyema.

Pia Mhe. Mtaka amewataka wananchi kujitokeza kushiriki zoezi la Sensa Agosti 23,2022 ili kupata takwimu sahihi kwa maendeleo ya nchi.

Naye Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa Dkt. Emmanuel Ishengoma ameeleza kuwa dhamira ya   wizara hiyo ni kuhakikisha  inafanya mageuzi  ya Sanaa na Utamaduni kwa kuwa ni Sekta muhimu  zinazotoa ajira kwa vijana na kuchangia katika uchumi wa nchi.

Tamasha la Cigogo linafanyika kwa siku tatu  Julai 22 hadi 24,2022 likiongozwa na Kauli Mbiu "Elimu ya Sanaa ni Muhimu kwa Maendeleo Endelevu " linapambwa na ngoma mbalimbali za kitamaduni kutoka kabila la Wagogo Dodoma.

MWISHO

Mwisho

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.