• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SENYAMULE AKEMEA UHARIBIFU WA MLIMA SAUNA -KONDOA

Imetumwa : February 9th, 2024

Ikiwa ni muendelezo wa ziara za kikazi za Ukaguzi wa Miradi ya maendeleo, kusikiliza na kutatua kero za wananchi na kukagua na kuhamasisha utunzaji endelevu wa mazingira kwa Halmashauri zote za Mkoa wa Dodoma Mhe. Senyamule amefika Wilayani Kondoa kujionea namna shughuli mbalimbali zinavotekelezwa Wilayani humo.

Akiwa Wilayani humo amewataka wananchi wa Kata ya Bereko hususani   Kijiji cha Kisese wanaofanya shughuli za kilimo katika mlima Sauna kupanda miti katika mashamba yao na kuachana na shughuli za kilimo na uchimbaji wa madini  Ujenzi katika mlima huo.

Senyamule ametoa maagizo hayo Februari 9/2023 alipofika kujionea  namna ambavyo mlima huo umeathiriwa na shughuli za mbalimbali za kibinadamu.

"Suala la kutunza mlima huu tulipe uzito na tusilete lelemama, viongozi wa hapa hakikisheni kila mtu anayelima katika eneo hili anapanda Miti kwenye shamba lake ndani ya wiki mbili ikiwa ni ishara kuwa mwaka huu ni wa mwisho kulima hapa na hatolima tena.

Aidha Mhe. Senyamule amewasihi wananchi wa Kata hiyo kutoa ushirikiano mzuri kwa viongozi ikiwemo kuwaainisha wote wanaojihusisha na masuala hayo katika hifadhi ya mlima huo.

"Kuna Siri muhimu za kuficha na Kuna nyingine ukizificha unapoteza uzalendo wako, hizi Siri mnazofichiana wanakisese hazitakiwi kufichwa kwasababu mnawaficha watu wanaoharibu mlima ambao unapoendelea kuharibiwa uasili wake unaweza kuleta madhara makubwa, niwasihi Kila mmoja awe kiongozi na mlinzi wa mwenzie ili mlinde mazingira yenu", amesema Senyamule.

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt. Khamis Mkanachi amesisitiza kuwa maelekezo ya  Mkuu wa Mkoa Mhe. Senyamule yanapaswa kufuatwa na kwamba serikali ya Kijiji imeondolewa kwenye usimamizi wa msitu huo.

Naye Kaimu Muhifadhi wa Misitu Wilaya ya Kondoa Bw. Amon Mgimwa amesema watasimamia sheria za Misitu na mazingira kulinda uoto wa eneo Hilo ikiwa ni pamoja na kufanya doria ya kuwasaka waharihifu na kuwachulia hatua Kali kwa mujibu wa sheria.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.