• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI IMEZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI VISHIKWAMBI KWA WALIMU NCHINI

Imetumwa : November 4th, 2022

Serikali imezindua zoezi la ugawaji vishikwambi kwa walimu nchini na kuzitaka Mamlaka zinazohusika na kazi hiyo kuhakikisha vishikwambi hivyo vinawafikia walengwa ili viweze kufanya kazi iliyokusudiwa.


Akizungumza Jijini Dodoma wakati wa uzinduzi huo Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amesema vishikwambi hivyo vinalenga kuboresha mchakato wa utoaji elimu ili kuinua ubora wa elimu nchini, hivyo ni vizuri vikawafikia walengwa ili lengo liweze kutimia.


“Hapa ningependa kusisitiza kuwa vishikwambi hivi ni kwa ajili ya walimu tu na si vinginevyo hivyo Viongozi wote wa Serikali mliopo OR- TAMISEMI, Halmashauri na wale wote watakaokuwa na jukumu la kugawa vishikwambi hivi hakikisheni hakuna mwalimu atakayekosa,” amesisitiza Mhe. Majaliwa.


Amesema Serikali ya Awamu ya Sita tangu kuingia madarakani imewekeza kwa kiasi kikubwa kwenye TEHAMA ikiwa ni utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2020 - 2025 ambayo inasisitiza matumizi ya TEHAMA katika ngazi mbalimbali za Elimu ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kuboresha maisha ya watu kwa ujumla.


“Walimu hakikisheni mnatumia vishikwambi hivi katika kuboresha mchakato wa utoaji elimu ili kuinua ubora wa elimu nchini na si vinginevyo na naamini mtahamasika katika kutumia TEHAMA katika ufundishaji na ujifunzaji,” ameongeza Mhe. Majaliwa.


Kwa upande wake Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Wizara ya Elimu imenunua jumla ya Vishikwambi 300,000 kwa lengo la kuendelea kuboresha mazingira ya ufundishaji na ujifunzaji nchini.


Amesema vishikwambi hivyo vinakwenda kurahisisha upatikanaji wa nyenzo za kufundishia na kujifunzia, kuongeza idadi ya walimu watakaotumia mfumo wa kujifunzia wa Taasisi ya Elimu Tanzania unaojulikana kwa jina la Learning Management System (LMS) na kuhama kutoka mfumo wa usahihishaji wa mitihani wa makaratasi kwenda mfumo wa usahihishaji wa mitihani kwa njia ya mtandao - (e-marking system).  


Mhe. Mkenda ametaja wanufaika wa vishikwambi hivyo na idadi zao kuwa ni Walimu wa shule za msingi za umma ambao watapatiwa 185,404, Walimu wa shule za Sekondari za umma 89,805; Wathibiti Ubora wa Shule ngazi ya Wilaya na Kanda 1,666, Wakufunzi wa vyuo vya Ualimu vya Umma 1,353 na Wakufunzi wa Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi (FDC)  297.


Wengine ni Maafisa Elimu ngazi ya Mkoa, Wilaya na Kata ambao watapatiwa vishikwambi  5,772,  Wakufunzi wa vyuo vya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi – VETA 996, na Baraza la Mitihani la Tanzania (NECTA) ambao watapatiwa vishikwambi 8,357.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MMUYA AHIMIZA UDHIBITI VIFO VYA MAMA NA MTOTO

    May 26, 2025
  • UHAKIKI ANUANI ZA MAKAZI KUANZA MEI 28 DODOMA

    May 26, 2025
  • WAWEKEZAJI WA VIWANDA KUTOKA DUBAI WABISHA HODI DODOMA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI KUTOKA TUME YA MADINI WAMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.