• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI KUENDELEA KUTATUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI DODOMA

Imetumwa : June 26th, 2023


Serikali ya Awamu ya Sita, inayoongozwa na Mhe Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kutatua changamoto mbalimbali ndani ya jiji la Dodoma kwa lengo la kuwawezesha wananchi kujikwamua kiuchumi. Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Daniel Chongolo katika viwanja vya Mtekelezo vilivyopo Shule ya Sekondari Central Jijini Dodoma.

akihitimisha ya ziara yake ya siku kumi ndani ya Mkoa wa Dodoma Ndugu Chongolo amesema kuwa changamoto hizo ni pamoja na migogoro ya ardhi,sekta ya kilimo, elimu, Maji na ubovu wa miundombinu ya kufika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya. Ndugu Chongolo amesema kuwa lengo la ziara yake mkoani humo ni ilikuwa ni kusikiliza wananchi wa Mkoa wa Dodoma na kutatua changamoto zao.

Vile vile amewaasa wafanyakazi wote waliopata nafasi za ajira kwenye miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa kufanya kazi kwa bidii ili kulinda ajira zaopamoja na kuacha tabia ya wizi na kuchukua vitu visivyo halali badala yake watangulize uzalendo mbele kwa maendeleo ya Mkoa na taifa kwa ujumla. Naye Naibu Waziri OR-TAMISEMI, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema barabara zinaendelea kuboreshwa na kutengewa fedha kwa ajili ya Ujenzi na kukamilishwa kwa Zahanati na Shule ya Sekondari. Aidha amesema kuwa changamoto za miundombinu ya Zahanati ya Chali iliyopo Wilaya ya Bahi, Kituo cha afya cha Msaada Wilayani Chemba vyote vitakamilishwa.

Kwa upande wake Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi Mhe. Dkt. Angelina Mabula amewataka wananchi wanaonunua ardhi kuanzia kwenye Halmashauri kabla ya kununua ili kupunguza migogoro ya ardhi na utapeliMheshimiwa Mabula amesema hayo wakati akijibu hoja kuhusu migogoro ya ardhiiliyopo ndani ya jiji la Dodoma kwani hadi sasa migogoro mingi ya ardhi imefanyiwa kazi na ipo kwenye ngazi za Kiutawala kwa ajili ya Uamuzi. Amesema kuwa Wizara yake imeweka Makamishina wawili wa ardhi maalumu, ambapo mmoja atashughulikia migogoro ya jiji na mwingine nje ya jiji.

Huku, Waziri wa Kilimo Hussein Bashe amesema kiwanda cha kuchakata zabibu kitajengwa na kitaendeshwa na sekta binafsi na viwanda vilivyopo ndani ya Mkoa wa Dodoma ikiwa ni pamoja na kuendelea kukamilisha skimu za umwagiliaji Mkoani Dodoma.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Rosemary Senyamule amesema ziara ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi imekukuwa na manufaa kwakuwa ameweza kupata elimu na kujifunza vitu mbalimbali sambamba na kuzifanyia kazi changamoto zilizojitokeza na kuahidi kuendelea kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi kikamilifu. .

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.