• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SERIKALI YAKABIDHIWA KITUO CHA AFYA ILAZO

Imetumwa : December 18th, 2024

Na Sofia Remmi

Habari-Dodoma Rs.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe.Rosemary Senyamule ameshiriki hafla ya Makabidhiano ya  Kituo cha afya  Ilazo  kilichojengwa Kwa ufadhili wa shirika la 'Korea International Cooperation Agency' ( KOICA) kwa kushirikiana na ' The United Nations Children's Fund ' ( UNICEF ).

Mashirika hayo yameikabidhi Serikali ya Mkoa kituo tayari kwa matumizi ya kuwahudumia Wananchi wa kata ya  Ilazo na maeneo jirani.

Akizungumza katika hafla hiyo Mhe. Senyamule amesema majengo hayo ya huduma za afya yamejengwa na kufadhiliwa na Shirika la la Korea KOICA Kupitia UNICEF.

“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ana lengo la kupunguza vifo vya kina mama wajawazito wakati wa kujifungua na watoto wachanga kwa kuleta huduma bora kwa wananchi wake kila kijiji na kila  mtaa.

“Uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi na mtoto imewezeshwa kwa kiasi kikubwa kwa kujenga vituo vya kutolea hiduma za afya, ununuzi wa dawa na  vifaa tiba kwenye kila halmashauri na kuwezesha Mkoa na kupokea kiasi cha shilingi Bilioni 34.51 kwa mwaka wa fedha 2022/23 na 2023/24 kwaajili ya uboreshaji wa miundombinu ya vituo vya huduma za afya na kiasi cha shilingi Billioni 34.20 kwaajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba, Mashine,” amesema Senyamule.

Kupitia fedha hizo zimejenga hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Bahi, Chemba, Chamwino, Kondoa na Dodoma Mjini, na kuweka mahusino mazuri baina ya  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Serikali ya Korea.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Dkt.Pima Sebastian amesema lengo la Mradi huu ni kuboresha huduma za Afya ya mama na Mtoto na huduma za upasuaji,  Mradi huu umeanza kutelelezwa mnamo tarehe 04/07/2023 na Ulikamilika 30/09/204.

“Mradi huu ulianza kutoa huduma tarehe 01/10/2024 na kupokea wateja/ wagonjwa  479 waliohudumiwa wakiwemo kina mama wajawazito na watoto chini ya Miaka mitano 212 na wagonjwa wa nje 267. kituo kina jumla ya watoa huduma 24 wakiwemo madaktari 05, wauguzi 10, wateknolojia maabara 02, wateknolojia dawa 02, wataalam watoa dawa za usingizi na gazi salama 02, tabibu meno 01, Katibu afya na Afisa lishe 01”

Hata hivyo Dkt. Sebastian amesema kituo hicho kimetumia  jumla ya shilingi Bilioni 3.2 hadi kukamilika kwake  kwaajili ya ujenzi na ununuzi wa vifaa tiba.

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.