• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TAARIFA KWA UMMA SERIKALI KUGHARIM MATBABU YA MAJERUHI NA MAZISHI YA WANAFUNZI WA AJALI -BAHI

Imetumwa : May 11th, 2023

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

OFISI YA RAIS

                     TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA

 
Mkoa wa Dodoma
Anwani ya Simu REGCOM
Simu Nambari: 2324343/2324384
E-Mail No. ras@dodoma.go.tz
Fax No. 255 026 2320046
 
 

 

     Ofisi ya Mkuu wa Mkoa,
       Jengo la Mkapa,
       2 Barabara ya Hospitali,
        S.L.P. 914,
        DODOMA.

11 Mei, 2023                                                                                                                               

TAARIFA KWA UMMA

SERIKALI KUGHARAMIA MATIBABU YA MAJERUHI NA MAZISHI YA WANAFUNZI WA AJALI- BAHI

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amesema Serikali itagharamia mazishi ya Wanafunzi wawili (2) wa shule ya sekondari  Mpalanga Wilayani Bahi waliofariki katika ajali ya gari iliyotokea leo majira ya saa 5:00 asubuhi katika Kijiji cha Chidilo  Wilayani humo.

Aidha, Mhe. Senyamule ameahidi kuwa, Serikali itagharamia matibabu ya wanafunzi wote majeruhi 31 walioumia katika ajali hiyo ambao wanaendelea kupatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.

Ajali hiyo imehusisha gari yenye namba za usajili T 519 BSY aina ya Mitsubishi Canter mali ya Bw. Abdul Rashid mkazi wa Dar es Salaam. Gari hiyo ilikuwa imebeba wanafunzi 51, walimu wawili na dereva mmoja ambao walikuwa wakielekea Shule ya Sekondari Magaga kushiriki mashindano ya michezo ya UMISETA

Kwa mujibu wa Mkuu wa Usalama barabarani Wilaya ya Bahi, ASP Bakari Ramadhani amesema kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa gari hilo lililobeba wanafunzi, uliosababisha gari kumshinda dereva, kuacha njia na kupinduka na hadi sasa dereva wa gari hiyo anashikiliwa na jeshi la polisi.

Akitoa salamu za Serikali Mhe. Senyamule amewataka wafiwa kuwa na moyo wa subra na kuelekeza Jeshi la Polisi kuchukua hatua haraka kwa wote watakaothibitika kuhusika na uzembe kwa namna yoyote ile.

"Ndugu zangu nawapa pole kwa niaba ya Mhe. Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan. Tumeguswa sana na misiba hii ya kupoteza nguvu kazi ya Taifa la leo na kesho. Serikali iko pamoja nanyi katika kipindi hiki kigumu, tutaendelea kushirikia katika wakati huu wa msiba kwa kusimamia mazishi ya marehemu na matibabu ya majeruhi wetu. Viongozi wote wakuu pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa ana Serikali za Mitaa (TAMISEMI) mwenye dhamana ya kusimamia Shule na Michezo mashuleni wanatoa pole sana ” Amesisitiza Mhe. Senyamule.

Awali Mhe. Senyamule amepata fursa ya kuwatembelea majeruhi 31 wanaoendelea na matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma huku Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dkt. Ernest Ibenzi akithibitisha kuendelea kuimarika kwa afya za majeruhi hao.

Pia, Mkuu wa Mkoa amepata fursa ya kutembelea familia zilizopatwa na misiba hiyo katika Kijiji cha Nholi na Chidilo. Waliofariki duniani ni Magreth Juma Shimba (18) mwanafunzi wa Kidato cha Nne ambaye anatarajiwa kusafirishwa kesho kuelekea Wilaya ya Kishapu, Shinyanga na Neema Yohana Hoya (16) mwanafunzi wa kidato cha pili atakayezikwa kesho Kijiji cha Chidilo, Wilayani Bahi.

IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI

 

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.