• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

“UTANGAZAJI: NGUZO YA MAADILI MEMA NA USALAMA WA NCHI “ - PROF. KABUDI

Imetumwa : February 13th, 2025

Na: Hellen M. Minja,

Habari - DODOMA RS

Kupitia malengo ya Utangazaji na vyombo vya Habari kwa ujumla ambayo ni kuhabarisha, kuelimisha na kuburudisha, Serikali Duniani zimekua zikitumia vyombo vya habari kuwasiliana na wananchi wake kuhusu Programu mbalimbali za Kitaifa na kuwahamasisha kushiriki katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Hayo yamebainishwa na Waziri mwenye dhamana ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi alipokua akizundua rasmi Mkutano wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji Nchini unaofanyika kwenye ukumbi wa 'New Generation' Jijini Dodoma.

Katika hotuba yake, Waziri Prof. Kabudi amesema; "Serikali nyingi Duniani zimekua zikitumia vyombo vya habari kuwasiliana na wananchi wake kuhusu Programu mbalimbali za Kitaifa na kuwahamasisha kushiriki miradi mbalimbali ya maendeleo. Hivyo, Redio ni chombo sahihi sana katika kufikisha habari kwa wananchi, kulinda maadili na usalama wa Nchi."

Kadhalika, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo ambaye pia ni Msemaji Mkuu wa Serikali Bw. Gerson Msigwa ameipongeza Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kwa kuandaa afua mbalimbali ambazo zinawasaidia Watangazaji wa leo kupata mazingira bora ya kufanya kazi zao kwa weledi.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Jabir Kuwe, amesema sekta ya Utangazaji imepitia mabadiliko makubwa kutokana na Teknolojia mpya kuingia sokoni hivyo Serikali kupitia TCRA imelazimika kufanya mabadiliko ya kanuni za Utangazaji mara kwa mara ili kukabiliana na changamoto za teknolojia hiyo.

Akitoa salamu za Mkoa wa Dodoma, Mkuu wa Mkoa huu Mhe. Rosemary Senyamule  amevishukuru Vyombo vya Habari kwa kutangaza na kuandika mambo mazuri ya Mkoa huu ambao ni Makao Makuu ya Nchi,hata ikasikika Duniani na kuifanya Dunia kuja kuwekeza Dodoma hivyo, ameahidi ushirikiano wa karibu kati ya Serikali ya Mkoa na Waandishi wa Habari.

Mkutano wa Mwaka wa Vyombo vya Utangazaji Nchini 2025, hufanyika kila mwaka sambamba na siku ya Redio Duniani ambayo inaenzi uasisi wa utangazaji ambao ulianzia kwenye chombo cha Redio ambapo baadae vilifuata vingine mpaka leo tunaposhuhudia teknolojia mpya kwenye tasnia ya Utangazaji.

Kauli mbiu: "Redio na mabadiliko ya tabia ya nchi".


#dodomafahariyawatanzania

#keroyakowajibuwangu

#birthdayyangumtiwangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • KAMPUNI YA "CAVO'' YA CHINA YATAFUTA FURSA ZA UWEKEZAJI DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.