• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

VETA YA SASA SI YA ZAMANI MATTAKA

Imetumwa : June 11th, 2024

Chuo cha mafunzo ya ufundi stadi (VETA) Kanda ya Kati, kimeimarika kwa sasa kufuatia uboreshaji wa mitaala inayokidhi teknolojia kutokana na ushindani wa soko la ajira. Hayo yamebainishwa na Kaimu Mkurugenzi wake Bw. Ramadhani Mattaka kwenye kipindi maalumu cha ‘Mitatu Dodoma na Samia’ kwa Taasisi za umma Mkoa wa Dodoma.

Kaimu Mkurugenzi huyo, ameipongeza Serikali kwa mafanikio makubwa ya VETA kwani imekua na utofauti mkubwa kutoka ile ya awali na hii ya kipindi hiki.

“VETA ya sasa si ya zamani. Serikali ya awamu ya sita imesaidia uboreshaji wa mitaala inayokwenda sambamba na mabadiliko ya teknolojia na ushindani wa soko la ajira nchini. Maboresho haya ni pamoja na kuongezeka kwa vifaa vya kisasa vinavyokidhi mitaala hii” Amesema Bw. Mattaka

Mafanikio mengine ambayo Serikali imeyafanya kwa Taasisi yake, amesema Serikali inachangia ada kwa wanafunzi wa bweni ambapo kila mwanafunzi analipia 120,000 kwa mwaka ambapo gharama halisi ni shilingi 900,000. Hivyo Serikali inatoa kiasi cha shilingi Bilioni 1.6 kwa ajili ya ada kila mwaka kwa vijana wa kitanzania.

Aidha, Serikali imetoa fedha zaidi ya Bilioni 12 kwa ajili ya upanuzi wa vyuo vya ufundi stadi Mkoa wa Dodoma ambapo kwa sasa itafikisha vyuo 7 kutoka chuo kimoja.

“Mkoa wa Dodoma ulikua na Chuo kimoja cha VETA lakini katika kipindi hiki, fedha zimetolewa takribani Bilioni 12 kwa ajili ya ujenzi wa vyuo vya VETA ambapo kila Wilaya itakua na chuo kimoja na ujenzi unaendelea. Hii inadhihirisha namna Rais anayodhamiria kutoa umasikini kupitia VETA” Bw. Mattaka.

Chuo cha ufundi stadi VETA kimeundwa kwa mujibu wa sheria za Tanzania mwaka 1994 kwa lengo la kutoa mafunzo ya ufundi stadi kutokana na wimbi la ukosefu wa ajira kwa vijana nchini. VETA kanda ya kati ni mojawapo ya Kanda 9 za vyuo hivyo ambapo kwa sasa ina vyuo 9 (Vitatu vya Mkoa na sita vya Wilaya huku ikihudumia mikoa Mitatu (Dodoma, Singida na Manyara).















Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.