• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

VIJANA NI RASILIMALI MUHIMU KWA TAIFA KUFIKIA MALENGO YA DIRA 2050

Imetumwa : August 12th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Vijana wanatajwa kuwa rasilimali muhimu inayotegemewa na Taifa katika kufikia malengo ya Dira 2050 iliyozinduliwa mwezi Julai 2025 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na watu wenye Ulemavu Bi. Zuhura Yunus alipokua akizungumza na vijana waliojitokeza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Vijana Kimataifa 2025 yaliyofanyika leo Agosti 12, 2025 kwenye ukumbi wa Mabelle uliopo Jijini Dodoma.

“Vijana ni rasilimali muhimu ambayo inategemewa na Taifa katika kufikia malengo na Dira ya Taifa 2050 ambayo imezinduliwa Julai 2025, natumai wote mmeshuhudia, ile hasa ni kwa ajili ya vizazi vyenu. Kuwawezesha vijana kushiriki kikamilifu katika kuchochea maendeleo ya jamii na Taifa ni suala la muhimu na lisiloepukika”. Bi. Yunus

Akitoa salamu za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma CPA. Eric Ntikahera amesema Taifa linawategemea vijana kwani ni nguvu kazi na tegemeo la maendeleo kulinga na Dira 2050 hivyo amewataka kuisoma na kuielewa kwani sehemu kubwa kama nchi inawategemea.

Nae Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Kimataifa (UNDP) Bw. Joseph Manirakiza, amesema maendeleo endelevu hayawezekani bila vijana kwani Miradi wanayoifanya kama Shirika, inalenga kufikia maendeleo endelevu kwa ajili yao hivyo, wametakiwa kutoa sauti na kutumia nguvu zao katika kulijenga Taifa.

Tanzania ikiwa ni Mwanachama hai wa Umoja wa Mataifa, inaungana na Jumuiya nyingine za Kimataifa kuadhimisha siku ya Vijana Kimataifa 2025 inayotambua na kuthamini mchango wa Vijana katika maendeleo ya jamiii, Taifa na Duniani kwa ujumla. Tanzania inaadhimisha siku hiyo chini ya kaulimbiu: “Nguvu kazi ya Vijana Tanzania, Kwa Maendeleo Endelevu”

#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MRADI WA ‘KOFFI’ WATOA DOLA BILIONI 2.455 KUBORESHA HUDUMA ZA UZAZI NA MTOTO DODOMA

    August 21, 2025
  • WANANCHI NA WADAU WAASWA KUCHAGIZA UTALII - DODOMA

    August 21, 2025
  • WADAU WAASWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA JAMII DHIDI YA MAJANGA

    August 19, 2025
  • WAFANYABIASHARA WA MKOA WA DODOMA WATANGAZIWA FURSA ZA BIASHARA NCHINI INDONESIA

    August 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.