• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

VIONGOZI WA SERIKALI WAASWA KUTEKELEZA DIRA 2025 ILI KUKUZA KILIMO IFIKAPO 2030

Imetumwa : August 1st, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Mwongozo mpya wa kuanzisha na kuendesha Shamba Darasa la Kilimo biashara uliozinduliwa leo Agosti Pili, 2025 na Wizara ya Kilimo kwa ufadhili wa Shirika la ‘Care International’ Tanzania, unatajwa kuwanufaisha Wakulima na Wadau wanaojihusisha kwa namna moja ama nyingine na shughuli za sekta ya kilimo.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Mweli wakati wa Kongamano la uzinduzi wa Mwongozo huo lililofanyika kwenye ukumbi iliopo ndani ya viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma katika Maonesho ya Nanenane Kitaifa 2025 Kanda ya Kati.

“Leo tunahitimisha mchakato wa kuandaa Mwongozo ili kuhakikisha huduma za ugani zinaendana na mahitaji ya sasa, mwongozo huu utawanufaisha wakulima, vyama vya ushirika, wataalam wa kilimo, taasisi za Umma na binafsi, kampuni za pembejeo, taasisi za fedha wabia wa maendeleo na wajasiriamali waliojipanga kuendeleza teknolojia mbalimbali za kilimo”  Bw. Mweli.

Aidha, Balozi wa Indonesia Nchini Tanzania Mhe. Tri Yogo Jatmiko aliyehudhuria Kongamano hilo amesema uchumi wa Taifa lake unategemea Kilimo na wanatumia teknolojia za kisasa kama kutengeneza mvua kupitia mawingu hivyo, hawategemei kilimo cha mvua za msimu na kufanya sekta hiyo kuwa na mchango wa 60% katika Pato la Taifa.

Akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Katibu Tawala Msaidizi Seksheni za Uchumi na uzalishaji Bi. Aziza Mumba, amesema wakati huu ambao Wizara inakwenda kutengeneza vituo vya zana za kilimo, izingatie changamoto wanayoipata wakulima hasa uwepo wa tabaka gumu la udongo linalozuia kutengeneza matuta ya kuhifadhia maji.

Vile vile, Mkurugenzi Mkaazi wa ‘Care International’ Tanzania Bi. Prudence Masako amesema Shirika lake linatekeleza miradi ya kilimo katika Mikoa ya Iringa, Mbeya, Njombe, Kigoma, Tanga, Shinyanga na Morogoro inayolenga wakulima wadogo hususan wanawake na vijana kwa lengo la kuwawezesha kutoka kilimo cha kujikimu hadi kilimo biashara.

Maonesho ya Nanenane 2025 yanaongozwa na Kaulimbiu: “Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelevu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi 2025” ambayo ni mahsusi ili kukumbusha umuhimu wa kuchagua viongozi bora katika kuinua uzalishaji kwenye sekta za Kilimo, Ufugaji na Uvuvi kipindi hiki Taifa linapoelekea kwenye Uchaguzi Mkuu, Oktoba 29, 2025.


 #dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MRADI WA ‘KOFFI’ WATOA DOLA BILIONI 2.455 KUBORESHA HUDUMA ZA UZAZI NA MTOTO DODOMA

    August 21, 2025
  • WANANCHI NA WADAU WAASWA KUCHAGIZA UTALII - DODOMA

    August 21, 2025
  • WADAU WAASWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA JAMII DHIDI YA MAJANGA

    August 19, 2025
  • WAFANYABIASHARA WA MKOA WA DODOMA WATANGAZIWA FURSA ZA BIASHARA NCHINI INDONESIA

    August 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.