• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

VYAMA VYA USHIRIKA VYAWANUFAISHA WAKULIMA KUPITIA MASOKO YA UHAKIKA YA MAZAO

Imetumwa : August 3rd, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Imabainishwa kuwa, Wakulima sasa wameanza kunufaika na uwepo wa soko la uhakika la mazao yao kupitia kujiunga kwenye vyama vya Ushirika kwani, Tani Milioni 3.8 za mazao mbalimbali yenye thamani ya shilingi Trilioni 6.2, zimeuzwa kupitia vyama hivyo vilivyoanzishwa kwa lengo la kuwasimamia Wakulima nchini.

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa, amebainisha hayo alipokua akizungumza na wadau pamoja na wanaushirika waliohudhuria Siku ya Ushirika leo Agosti Tatu, 2025 kwenye Kijiji cha Ushirika kinachopatikana ndani ya Maonesho ya Nanenane Kitaifa 2025 Kanda ya Kati katika viwanja vya Nzuguni Jijini Dodoma.

“Tani Milioni 3.8 za Mazao mbalimbali ya yenye thamani ya shilingi Trilioni 6.2 zimeuzwa kupitia vyama vyetu vya Ushirika tulivyo navyo, hii ina maana kwamba Wakulima wameanza kupata masoko mazuri ya uhakika, bei nzuri kwenye masoko yetu na tumepanua wigo wa masoko hivi sasa ili Mkulima awe na uhakika na zao lake kupata soko”.

Aidha, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amesema kuwa Mkoa wake pia una mazao ambayo wakulima wake wamejiunga kwenye vyama vya Ushirika hivyo wanapata masoko ya uhakika wakiuza kupitia Mfumo wa Stakabadhi ghalani.

“Mkoa wa Dodoma tuna mazao ambayo yamejiunga katika Ushirika, tuna Korosho pale Kongwa na Mpwapwa ambazo wanazalisha kwa kiasi kikubwa na wana chama cha Ushirika ambacho kinauza kwa njia ya Stakabadhi ghalani lakini pia tuna Zabibu ambayo pia ina chama cha Ushirika”.

Hata hivyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo Bw. Gerald Mweli, amesema maono ya Wizara yake kwa niaba ya Serikali, ni kuhakikisha vyama vya Ushirika ambavyo vinajishughulisha na uzalishaji, vinaanzia kwenye uzalishaji hadi sokoni kama ilivyo kwenye mazao ya Pamba na Korosho ambayo yanauzwa moja kwa moja kwenye masoko ya Kimataifa.

Nae, Mrajisi wa vyama vya Ushirika Dkt. Benson Ndyege amesema mali za ushirika zilizorudishwa ikiwa ni pamoja na viwanda, zimeanza kufanya kazi na kuwanufaisha wanaushirika na watanzania kwa ujumla na sasa wameleta utaratibu wa kuzitambua kidijitali ambapo wameshatambua mali 4,990 za ushirika zenye thamani ya takribani shilingi Trilioni 1 na mahali zilipo.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MRADI WA ‘KOFFI’ WATOA DOLA BILIONI 2.455 KUBORESHA HUDUMA ZA UZAZI NA MTOTO DODOMA

    August 21, 2025
  • WANANCHI NA WADAU WAASWA KUCHAGIZA UTALII - DODOMA

    August 21, 2025
  • WADAU WAASWA KUSHIRIKIANA NA SERIKALI KUJENGA JAMII DHIDI YA MAJANGA

    August 19, 2025
  • WAFANYABIASHARA WA MKOA WA DODOMA WATANGAZIWA FURSA ZA BIASHARA NCHINI INDONESIA

    August 15, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.