• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAKANDARASI WASIOKAMILISHA MIRADI KUDAIWA FIDIA

Imetumwa : May 21st, 2025

Na. Sizah Kangalawe - Dodoma Rs

Waziri wa Ujenzi Mhe. Abdallah Ulega, amewataka Wakala wa  Barabara Nchini (TANROADS) na Taasisi nyingine zinazosimamia ujenzi wa miradi ya Serikali, kuwatoza faini wakandarasi wanaochelewa kukamilisha miradi hiyo baada ya mikataba yao kumalizika, ikiwa wameshapatiwa stahiki zao zote.

Agizo hilo limetolewa na Waziri huyo wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi mbalimbali  inayotekelezwa na Wizara hiyo kupitia kupitia TANROADS  Mei 21/2025 Jijini Dodoma.

‘’Hakikisheni tunawadai kwasababu sisi tumekuwa tukidaiwa kwenye miradi yetu pindi tukichelewesha jambo, kwahiyo inapotokea wao wamechelewa ni lazima na wao watulipe sisi  kwa muda ambao wamechelewa, kama msumeno vile, unakata pande zote kwetu na kwao.

Aidha Mhe. Ulega ameitaka TANROADS kushirikiana kwa karibu na Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) ili kurahisisha utendaji kazi kwani baada ya kumalizika kwa ujenzi huo Mradi utakabidhiwa kwa TAA.

‘’TANROADS na TAA mpo hakikisheni  mnashirikiana kwa karibu kufanya hii kazi, hili jambo ni la Watanzania wote, ni kweli kazi ya ujenzi tumepewa sisi TANROADS na Mikataba yote lakini TAA ndio watumiaji na Watanzania wote, TAA akiona uzito wa mambo ninyi msimfungie milango kuona kwamba hawezi kutoa ushauri, msukumo. Inawezekana kuna jambo atakaloliona yeye kama mtumiaji , msimamizi wa baadae mradi ukikamilika, mkifunga milango atashindwa kuwashauri kitaalamu’’, Ameagiza Ulega

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amewaomba Wizara ya Ujenzi kwa kushirikiana na TRC kujenga njia ya mchepuko ya muda ili kuwezesha bandari kavu kuanza kufanya kazi yake kama ilivyokusudiwa wakati ujenzi wa barabara kuu ukiendelea.

Ziara hiyo imehusisha kutembelea barabara ya mzunguko wa nje kutoka Ihumwa – Matumbulu na Matumbulu- Veyula ambapo ujenzi wake unatarajiwa kukamilika kati ya Julai 31 na Agosti 30/2025, Ujenzi wa Uwanja wa ndege wa kimataifa Msalato ambao utakuwa na uwezo wa kusafirisha abiria Milioni moja na laki tano kwa mwaka pamoja kuwa na uwezo wa kuegesha ndege 17 kwa wakati mmoja.

Hata hivyo miongoni mwa maagizo yaliyotolewa katika ziara hiyo ni pamoja na wakandarasi kufanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha miradi kwa wakati na kuzingatia mahitaji ya watumiaji wadogo wa barabara pindi wanapojenga barabara ya juu ( Fly over) katika makutano ya barabara ya juu ya mzunguko wa nje Mtumba, jijini Dodoma.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawidhadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MMUYA AHIMIZA UDHIBITI VIFO VYA MAMA NA MTOTO

    May 26, 2025
  • UHAKIKI ANUANI ZA MAKAZI KUANZA MEI 28 DODOMA

    May 26, 2025
  • WAWEKEZAJI WA VIWANDA KUTOKA DUBAI WABISHA HODI DODOMA

    May 28, 2025
  • VIONGOZI KUTOKA TUME YA MADINI WAMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 28, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.