• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WANAWAKE WAOMBOLEZAO KUKUTANISHWA KWENYE KONGAMANO KULIOMBEA TAIFA DODOMA

Imetumwa : July 16th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Katika kipindi hiki ambacho Taifa linaelekea kwenye uchaguzi Mkuu wa Viongozi wa Serikali, Wanawake waombolezao watakutanishwa katika Kongamano la siku tatu la maombi kwa kuwa wana kina cha maombi kinachowezesha nchi kuwa na Amani, kwani bila Amani hakuna jambo la maendeleo litakaloweza kufanyika.

Hayo yamesemwa na Mchungaji wa Kanisa la ‘Tanzania Fellowship of Churches’ Deborah Godfrey Malassy ambaye Kanisa lake limeandaa Kongamano la 16 la Wanawake waombolezao Kitaifa alipokua akizungumza kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari uliofanyika kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Julai 16, 2025.

“Wanawake waombolezao wana kina cha maombi kwa ajili ya Taifa letu, kama mnavyojua katika kipindi hiki cha uchaguzi mbele yetu, kuna watoto, familia, uchumi na mambo mengine, tunawakutanisha kina Mama kuomba na kuomboleza kwa ajili ya kuweka hali nzuri ya Amani kwani nchi bila Amani hatuwezi kukaa”

Kadhalika, hakuna kiingilio katika kushiriki Kongamano hilo litakaloongozwa na Mnenaji Mkuu Katherine Kahabi huku wengine wakiwa Mwalimu Wilbroad Prosper, Mwalimu Miriam Mulokozi, Mchungaji Deborah Kaisi na wenyeji Askofu Dkt. Godfrey Emmanuel Malassy pamoja na Mchungaji Deborah Malassy.

Mgeni rasmi katika Kongamano hilo siku ya ufunguzi anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. George Simbachawene huku siku ya kufunga akitarajiwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule.

Kongamamo hilo lilianza rasmi mwaka 2009 na hufanyika mara moja kwa mwaka likitokana na Mkesha mkubwa wa Dua maalum ambao hufanyika Desemba 31 kila mwaka, na mwaka huu linatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere, ndani ya Chuo cha Mipango Jijini Dodoma kuanzia tarehe 18 hadi 20 Julai, 2025.

Neno litakaloongoza Kongamano ni; YEREMIA 9:17-21

#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WABAPTIST KUJENGA MAKAO MAKUU YAO DODOMA

    July 16, 2025
  • WANAWAKE WAOMBOLEZAO KUKUTANISHWA KWENYE KONGAMANO KULIOMBEA TAIFA DODOMA

    July 16, 2025
  • SERIKALI IMEJIPANGA KUHAKIKISHA WAFANYABIASHARA WANAKUWA NA MAZINGIRA RAFIKI

    July 14, 2025
  • MZUMBE MBIONI KUANZA KAMPASI DODOMA

    July 14, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.