• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WATANZANIA WAASWA KUTUNZA TUNU AMANI KUELEKEA UCHAGUZI MKUU

Imetumwa : July 11th, 2025

Na Sofia Remmi,

Dodoma-Habari Rs

Watanzania wametakiwa kuendelea kuitunza Tunu ya amani wakati nchi ikielekea kwenye zoezi la Kitaifa la uchaguzi mkuu huku  Wanasiasa wakitakiwa kufanya kampeni za kistaarabu ambazo hazichochei hasira na vurugu zisizo na tija.

Mwenyekiti wa kamati ya maridhiano Mkoa Askofu Dkt. Venance Chande, ameyasema hayo leo Tarehe 11 Julai 2025, wakati wa Mkutano wa kutoa taarifa ya Kongamano lililoandaliwa na Idara ya Elimu ya Mahakama ya Kadhi na Baraza la Waislam Tanzania (BAKWATA) kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma.

Askofu huyo amesema kuwa amani ndio msingi wa maendeleo ya Taifa lolote Duniani.

"Sisi Watanzania hatujazoea kugombana, tumezoea kuishi pamoja  kwa umoja na upendo, hatujazoea kubaguana kwa misingi ya makabila au dini zetu, hayo ndiyo maisha tuliyoyazoea kuishi".

Aidha, amewataka Wanasiasa kufanya siasa za kistaarabu.

"Wanasiasa, huu ni mwaka wa uchaguzi kampeni zifanyike kistaarabu zisiwe za kuchochea hasira, washawishi kwa Sera, tupingane kwa hoja na si kwa kuchochea vurugu zisizokuwa na tija kwa Taifa" Dkt. Chande

Kwa upande wake, Naibu Kadhi Shekhe Ally Nguruko, amesema kuwa lengo la kongamano hilo ni kujadili hatma ya nchi katika suala zima la amani kuelekea uchaguzi mkuu

vilevile mesema kuwa Kongamano hilo litakuwa la pili ambapo la kwanza lilifanyika Jijini Dar es salaam na linabeba kauli mbiu ya "Amani Yetu, Taifa Letu".

Ameongeza kuwa, miongoni mwa Mada zitakazotolewa katika ni pamoja na, athari za mitandao katika kuchangia kuharibika kwa amani, Afya duni ya akili na nyinginezo.

Aidha Kongamano hilo litakalofanyika Julai 13, 2025 katika ukumbi wa Sephil Sepphire Jijini hapa, linatarajiwa kufunguliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule na kufungwa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • SERIKALI IMEJIPANGA KUHAKIKISHA WAFANYABIASHARA WANAKUWA NA MAZINGIRA RAFIKI

    July 14, 2025
  • MZUMBE MBIONI KUANZA KAMPASI DODOMA

    July 14, 2025
  • AMANI YA NCHI YATAJWA KUWA AJENDA YA VIONGOZI WA SERIKALI NA WADINI

    July 13, 2025
  • DODOMA KUONDOKANA NA UKAME KUTOKANA NA UWEKEZAJI KATIKA MIRADI MIKUBWA YA UMWAGILIAJI

    July 13, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.