Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe Anthony Mtaka, ameyazungumza hayo hivi karibuni mara baada ya kualikwa kuwa Mgeni rasmi katika hafla ya kuwapongeza na kuwapatia vyeti wanafunzi wa shule za msingi za Kanda ya kati (Singida na Dodoma) walioshiriki katika mashindano ya uandishi wa Insha yaliyoandaliwa na Shirika la Kimataifa la World Vision katika ukumbi wa St. Gasper Jijini Dodoma.
Akizungumza Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe.Mtaka ametoa nasaha kwa wazazi na wanafunzi waliofanya vizuri katika mashindano hayo kuwa imefika wakati Sasa, tuangalie Elimu yetu ya msingi iwe kuanzia darasa la kwanza mpaka kidato cha Nne. "Natamani watoto wote wa shule za msingi na sekondari waweze kushiriki katika mashindano haya pindi yatakapoanza tena".Amesisitiza Mhe. Mtaka
Kwa mujibu wa mratibu wa kampeni ya kupinga ndoa na mimba za utotoni kutoka Shirika la World Vision Bw. Geoffrey Kisemba, ameeleza lengo kuu la mashindano hayo ni kuwajengea watoto uwezo wa kutoa mawazo yao katika kupinga suala la mimba za utotoni, ambapo takribani wanafunzi 3,600 kutoka shule 46 za Kanda ya kati walishiriki na leo washindi wanapokea zawadi zao za fedha taslimu, vyeti pamoja na baiskeli.
MWISHO
Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa
Anuani ya Posta: 914 DODOMA
Simu: +255 26 232 4343/232
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz
Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.