• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAZAZI WASISITIZWA KUPELEKA WATOTO SHULE KUFUATIA KUIMARIKA KWA MIUNDOMBINU YA ELIMU

Imetumwa : May 8th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Msisitizo unazidi kutolewa kwa wazazi wa Mkoa wa Dodoma juu ya umuhimu wa kuwapekeka watoto wao shule kwani Serikali ya awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan imewekeza fedha nyingi kwenye ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya elimu katika Mkoa huu.

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipokua akizungumza na wakazi wa Kata ya Paranga, Halmashauri ya Wilaya ya Chemba Mei 08, 2025 katika Mkutano wa hadhara mara baada ya kutembelea na kukagua miundombinu ya shule na mabweni katika baadhi ya shule zilizopo Wilayani humo.

“Chemba ni moja ya Wilaya ambayo inatuvuta nyuma kwenye matokeo ya Mitihani ya mwisho. Kwa hiyo, kwenye elimu tusifanye mchezo, lindaneni wenyewe, hakikisha mtoto anakwenda shule, manufaa yake mtayaona, elimu inalipa wala haichelewi”. Amesisitiza Mhe. Senyamule.

Licha ya suala la elimu, Mhe. Senyamule amewahimiza wakati hao kuhusu suala la uchumi kupitia kilimo cha matunda hususan Matufaha (Apples) kwani utafiti umefanyika na kuonekana yanafanya vizuri katika ardhi ya Dodoma pia yana soko kubwa hivyo, matamanio ya Serikali ya Mkoa ni kuona mabadiliko ya uchumi kwa wananchi wake.

Akizungumza katika hadhara hiyo kabla ya kumkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Chemba Mhe. Halima Okash, amesema Serikali imefanya kazi kubwa kwa kuwekeza fedha nyingi katika Kata hiyo ambapo zaidi ya shilingi Bilioni 11.5 kwenye miradi ya Maji, Milioni 60 kwa ajili ya Maabara mbili, madarasa yenye thamani ya zaidi ya Milioni 360.

Miradi iliyotembelewa na Mkuu wa Mkoa ni pamoja na ujenzi wa shule ya wavulana ya Kanda ambayo inagharimu kiasi cha shilingi Bilioni 4.6 kupitia mpango wa kuboresha elimu (SEQUIP) na inatarajiwa kukamilika June 2025 ambapo mradi huo unalenga kutoa elimu kwa wanafunzi 960 wa kanda ya kati kwa ngazi ya O-level na A-level .

Ujenzi wa Bweni katika shule ya Sekondari Mrijo unaotekelezwa kwa fedha za Serikali kuu kupitia EP4R, mapato ya ndani na nguvu za wananchi ambapo unagharimu kiasi cha shilingi Milioni 214.4, Mradi wa ujenzi wa Hosteli katika shule ya Sekondari Jangalo unaogharimu kiasi cha Shilingi Milioni 144.4

Lengo la ujenzi wa Mabweni na Hosteli katika shule hizo ni kupatikana kwa elimu bora kwa wanafunzi wa Kata hizo, kupunguza changamoto za wanafunzi kutembea umbali mrefu kufika shuleni, kutoa nafasi ya elimu bora pamoja na kupunguza adha na madhila wanayopata hasa wasichana kutoka kwa vijana wa mtaani maarufu kama ‘maronjoo’.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WAZAZI WASISITIZWA KUPELEKA WATOTO SHULE KUFUATIA KUIMARIKA KWA MIUNDOMBINU YA ELIMU

    May 08, 2025
  • WATUMISHI HODARI 2025 KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA WAPONGEZWA

    May 09, 2025
  • MRADI WA KUIMARISHA HUDUMA ZA KIFAFA WAZINDULIWA DODOMA

    May 08, 2025
  • UBALOZI WA UINGEREZA NCHINI TANZANIA WAADHIMISHA MAFANIKIO YA MWAKA MMOJA NCHINI

    May 08, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.