• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WIZARA TAFUTENI SULUHU YA MBWA WOTE WANAOZURURA MITAANI"-MHE.SENYAMULE

Imetumwa : September 28th, 2022


Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule alipokuwa akizindua maadhimisho ya utoaji chanjo kwa mbwa na ili  kujikinga dhidi ya ugonjwa wa kichaa cha mbwa yaliyofanyika katika viwanja vya Mpunguzi Jijini Dodoma.

“Kila mtu ambaye anafuga mbwa lazima afuate sheria na taratibu zake, naagiza wataalamu wa mifugo wa Wizara na Sekretarieti kutafuta suluhu ya mbwa wote wanaozurura mitaani. Mtu kama hawezi kufuata sheria, aache kufuga wanyama hao”  Amesema Mhe. Senyamule

Mkuu wa Mkoa ameeleza, ugonjwa wa kichaa cha mbwa husababisha vifo 1500 kila mwaka nchini na Watoto chini ya miaka mitano ndio wamekuwa wahanga wakubwa zaidi. Hivyo, Serikali inatekeleza mpango mkakati wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi katika kutoa chanjo hii kila mwaka ambapo mpaka sasa takribani mbwa 338,000 wameshachanjwa.

Mhe. Senyamule ametaja  lengo la Dunia ni kutokomeza ugonjwa wa kichaa cha mbwa ifikapo mwaka 2030 kwa kuhakikisha kuwa kila mbwa anapatiwa chanjo kila mwaka. “Naomba utaratibu huu uwe endelevu mpaka ugonjwa huu uwe historia kwani Tanzania bila kichaa cha mbwa, inawezekana. Tunatakiwa kuzingatia chanjo pamoja na kupunguza idadi ya mbwa tunaofuga” Amesisitiza Mhe. Senyamule

Naye Mkurugenzi wa huduma za mifugo Profesa Hezron Nonga, amesema nchini Tanzania tuna mbwa takribani milioni 4.5 na paka milioni 2 wanaofugwa kwa malengo mbalimbali na kwa mwaka kuna wastani wa matukio 2,030 ya mbwa wanaodhaniwa kuwa na kichaa. Hivyo Shirika la Afya Dunia (WHO), Shirika la Afya za Wanyama duniani (WOAH) na Shirika la chakula na kilimo (FAO) kwa pamoja wamekubaliana kutokomeza ugonjwa wa kichaa cha mbwa ifikapo mwaka 2030.

“Takwimu zinaonyesha kuwa watu zaidi ya 60,000 hupoteza Maisha kwa kichaa cha mbwa duniani kila mwaka. Kwa Tanzania, kila mwaka wastani wa matukio ya majeraha kwa binadamu yanayotokana na kuumwa na mbwa ni 3,387 na hiin ni kwa mujibu wa ripoti ya WHO ya mwaka 2017.  Ugonjwa huu husababisha wastani wa vifo vya binadamu 1500 kila mwaka” Prof. Nonga

Maadhimisho ya utoaji chanjo kwa mbwa na paka hufanyika kila mwaka Duniani ikiwa ni kumuenzi muasisi wake Dr. Luis Paster ambaye ndiye aligundua chanjo hii kwa wanadamu na mbwa kwa mara ya kwanza mwaka 1885. Maadhimisho haya yanakwenda sambamba na utoaji wa chanjo ambapo kwa mwaka huu chanjo zaidi  ya 60,000 zenye thamani ya shilingi Milioni 180 zimetolewa, lengo ni kuchanja mbwa kwa zaidi ya asilimia 70.

Aidha, maadhimisho ya mwaka huu yamebebwa na kauli mbiu inayosema, “Kichaa cha mbwa, afya moja, vifo sifuri” ikiwa na lengo la kutokomeza kabisa vifo vya binadamu vinavyotokana na ugonjwa wa kichaa cha mbwa.

MWISHO

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MADEREVA WA SERIKALI WATAKIWA KUZINGATIA SHERIA ZA USALAMA BARABARANI

    May 17, 2025
  • WATANZANIA WATAKIWA KUILINDA NA KUIDUMISHA AMANI NI KURUHUSU MAENDELEO NCHINI

    May 15, 2025
  • MKURUGENZI WA ‘WATER FOR PEOPLE ‘ AMTEMBELEA RAS MMUYA

    May 16, 2025
  • WANAFUNZI KIDATO CHA SITA WAASWA SAFARI YA ELIMU BADO NI NDEFU

    May 17, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.