• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

DIRA 2050 YALENGA KUFIKIA UCHUMI WA KATI WA JUU WA DOLA TRILIONI MOJA NCHINI

Imetumwa : July 17th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Tume ya Taifa ya Mipango kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Mpango wa muda mrefu unaoandaliwa, imeelekezwa kuandaa nyenzo zitakazotumika kupima matokeo ya utendeji Serikalini kwa kuzingatia malengo na Shabaha ya Dira 2050 inayolenga kufikia uchumi wa kati wa juu wa Dola Trilioni moja kabla ya kuanza kutumika kwa Dira hiyo.

Maelekezo hayo yametolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati wa hafla ya Uzindunzi wa Dira 2050 iliyofanyika Julai 17, 2025 kwenye ukumbi wa Kituo cha Mikutano  cha Jakaya Kikwete, Jijini Dodoma.

“Dira 2050 imeweka lengo na shabaha kubwa kufikia uchumi wa kati wa juu wa Dola Trilioni moja, ni wazi hatutaweza kufikia lengo hili kama tutaendelea kufanya kazi kimazoea, naelekeza Tume ya Mipango kwa kushirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu pamoja na Mpango unaoandaliwa, waweze kuandaa kwa haraka nyenzo zitakazotumika kupima utendaji Serikalini kwa kuzingatia malengo na shabaha za Dira hii kabla ya kuanza kutumika”.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha Mhe. Rais, Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Philip Mpango, amesema Dira ya Taifa inachochea matumaini na kuhamasisha Wananchi kuchukua hatua huku ikiongoza maamuzi ya kisera na hatimaye kuumba mwenendo wa maendeleo ya Nchi, hivyo kuunganisha nguvu za raia kuelekea katika malengo ya pamoja.

Kadhalika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Mipango na Uwekezaji Mhe. Prof. Kitila Mkumbo, ametaja malengo mahsusi ya Dira 2050 kuwa ni, Tanzania kufikia hadhi ya uchumi wa kipato cha kati ngazi ya juu ambayo kwa mujibu wa Benki ya Dunia, Pato la Taifa kwa mtu mmoja lina thamani ya Dola za Kimarekani kati ya 4,516 na 14,005.

Aidha, Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Mipango Dkt. David Msemwa, amesema ukusanyaji wa maoni ya wananchi juu ya uundwaji wa Dira hiyo, ulifanikiwa kuwafikia Watanzania 1,174,000 waliotoa maoni ya ‘ana kwa ana’ huku waliotuma jumbe fupi kwa njia ya simu wakiwa zaidi ya 8000, Mitandao ya kijamii zaidi ya 100,000 kupitia Mikutano, Makongamano na Semina Watanzania zaidi ya 22,000 walishiriki.

Akitoa salamu za Mkoa, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ametoa tathmini ya utekelezaji wa Mpango huo huku akimpongeza Mhe. Rais kwa kufanikisha yale yaliyokuwepo kwenye Mipango ya nyuma.

“Mpango huu ambao unakwenda kuuzindua leo, tayari unatuonesha mafanikio 60% ya utekelezaji wake, kazi tunayobaki nayo sasa ni 40% kwa kazi kubwa na nzuri ambayo umeifanya. Mhe. Rais umeonesha uzalendo mkubwa kwa kutekeleza mambo yaliyokuwepo na yaliyokua kwenye mipango ya miaka ya nyuma sana.”


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • VIJANA RIKA BALEHE 13,218 MKOA WA DODOMA WANUFAIKA NA UTEKELEZAJI WA MRADI WA AHADI

    July 23, 2025
  • MAAMBUKI YA UGONJWA WA HOMA YA INI ‘B’ YAFIKA 3.5% KITAIFA

    July 24, 2025
  • DODOMA NBC MARATHON YALENGA KUOKOA MAISHA YA MAMA NA MTOTO

    July 24, 2025
  • NGO’s DODOMA ZATAKIWA KUWAJIBIKA KWA SHERIA NA TARATIBU

    July 23, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.