• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Kongwa

Historia ya Kongwa

Utangulizi:

Halmashauriya Wilaya ya Kongwa ni miongoni mwa wilaya saba (7) za mkoa wa Dodoma, ilianzishwa mwaka1996 chini ya sheria  ya Serikali za Mitaa ya mwaka 1982 kifungu Na. 8 naNa. 9. Wilaya ina ukubwa wa eneo la kilometa za mraba 4,041 ambapo eneo linalofaa kwa kilimo naufugaji ni hekta 363,690.Wilaya ina Tarafa 3 za Kongwa, Mlali na Zoissa, Kata 22, Vijiji 87,Vitongoji 383 naMamlaka za miji midogo miwili ya Kongwa na Kibaigwa. Wilaya imepakana na Wilayaya Chamwino upande wa Magharibi; Wilaya ya Gairo (Mkoa wa Morogoro), upande waMashariki; Wilaya ya Mpwapwa upande wa Kusini na kwa upande wa Kaskazini kuna Wilaya ya Kiteto (Mkoa wa Manyara).

Kwa mujibu wasensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Wilayaina ongezeko la watu laasilimia 2.4; Hivyokwa mwaka 2015 wilayaya Kongwa inakadiriwa kuwa na jumla ya  watu 332,831 ambapowanaume ni 160,225 na wanawake ni 172,606. Aidha,Idadi ya kaya zilizopo kwa sasa ni 61,994. Kaya zinazojihusisha na shughuli za kilimo pamoja na ufugaji ni 55,573 sawa na  90%. 

Wenyeji wa Wilaya hii ni Wagogo, Wakaguru, na Warangi. Pia kuna makabila mengine ambayo yalihamia toka sehemu mbambali za Tanzania kama vile Wabena, Wanguu, Wakamba na Wamasai ambao walikuja kwa ajili ya shughuli za kilimo na mifugo.

Shughuli kuu za kiuchumu zinazofanywa na wakazi wa Wilaya ya Kongwa ni ufugaji wanyama (ng’ombe, mbuzi, kondoo, na punda). Punda hutumika zaidi katika usafirishaji wa mazao. Pia shughuli za kilimo cha mazao ya chakula na biashara mfano mahindi, mtama, uwele, karanga na alizeti.

Kujulikana kwa Kongwa:

Wilaya ya Kongwa lianza kujulikana katika ramani ya Dunia mwaka 1913 ambapo Shirika la Kidini kutoka Canada ambalo lilijulikana kama Church Missionary Society walipoanza ujenzi wa Chuo cha Ualimu na Theolojia mwaka 1909 katika kijiji cha Mlanga. Lakini kutokana na Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia, ujenzi huo ulichukua muda mrefu hivyo kukamilika mwaka 1927. Vifaa vilivyotumika katika kujengea Chuo hicho ni mawe na chokaa iliyochomwa.

Chuo kilifundisha taaluma ya Uchungaji (Theolojia), Ualimu na Uuguzi. Wanafunzi waliosoma katika Chuo hicho walitoka sehemu mbalimbali za Tanganyika na Kenya. Miongoni mwa wanafunzi wa kwanza waliosoma katika Chuo hicho ni Mzee Musa Fungo na Yohana Malecela.

Wakati wa vita ya Wakoloni baina ya Waingereza na Wajerumani mwaka 1914 – 1918, wanafunzi 12 walisoma katika Chuo hicho walikamatwa na Wajerumani na kupelekwa Zanzibar kuhifadhiwa na vita ilipoisha walirudishwa. Wakazi wengi walioishi katika eneo la Mlanga, wengi wao ni wahamiaji toka sehemu za Berege (Morogoro), Tanga na Iringa na Kiongozi wao kwa kipindi hicho alikuwa anaitwa Chifu Mahinyila. Katika eneo la Mlanga karibu na mlima kuna alama za miguu ya Farasi ambao walipitishwa katika njia hiyo na Wakoloni wakati wa vita.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2020 January 15, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 SHULE ZA BWENI (WASICHANA NA WANAUME) . December 20, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KIWANDA CHA AINA YAKE KUJENGWA KONGWA

    March 17, 2023
  • WAFANYAKAZI WAASWA MSHIKAMANO MAHALA PA KAZI

    March 15, 2023
  • BILIONI 4.6 KUIBADILISHA RANCHI YA KONGWA

    March 15, 2023
  • SENYAMULE AWAKARIBISHA MABALOZI DODOMA

    March 15, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Mkoa akiongoza siku ya maombi jijini Dodoma
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.