• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

RAIS MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA LAMI YA DODOMA-BABATI KM 251

Imetumwa : April 27th, 2018

RAIS MAGUFULI AFUNGUA BARABARA YA LAMI YA DODOMA - BABATI (KM 251)

(Habari na Ikulu)

Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo Aprili 27, 2018 amefungua barabara ya Lami ya Dodoma-Babati yenye urefu wa Kilometa 251 ambayo imekamilisha ujenzi wa lami katika barabara kuu ya kaskazini iitwayo “The Great North Road” ambayo inaanzia Cape Town nchini Afrika Kusini hadi Cairo nchini Misri.

Sherehe za Ufunguzi wa barabara hiyo zimefanyika katika eneo la Bicha, wilaya ya Kondoa mkoani Dodoma na kuhudhuriwa na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Akinumwi Adesina na Balozi wa Japan hapa nchini Mhe. Masaharu Yoshida.

Akitoa taarifa ya mradi huo Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mhandisi Patrick Mfugale amesema kazi za ujenzi ziligawanywa katika sehemu 4 ambazo ni Dodoma-Mayamaya (km 43.65), Mayamaya-Mela (km99.35), Mela-Bonga (km88.8), Babati-Bonga (km16.2) na km 3 za kuingia Kondoa Mjini, na kwamba mradi huo umegharimu shilingi Bilioni 378.4.

Rais wa Benki ya AfDB ambayo imetoa mkopo wa shilingi Bilioni 203.14 kuchangia ujenzi huo Dkt. Adesina ameelezea kufurahishwa kwake na kukamilika kwa barabara hiyo na kubainisha kuwa itasaidia kukuza biashara, Utalii, kuunganisha familia na kuimarisha utangamano wa nchi za Afrika.

Dkt. Adesina amempongeza Mhe. Rais Magufuli kwa juhudi zake za kufuatilia upatikanaji wa fedha za miradi kutoka AfDB tangu akiwa Waziri wa Ujenzi, na amesisitiza kuwa AfDB itaendelea kuunga mkono juhudi zake za kuwaletea Maendeleo Watanzania ikiwemo kujenga Miundombinu ya Jiji la Dodoma.

Akizungumza kabla ya kufungua barabara hiyo Rais Magufuli ameishukuru AfDB na Serikali ya Japan kupitia Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kwa ufadhili wake katika ujenzi wa barabara ya Dodoma-Babati pamoja na miradi mingine hapa nchini.

Mhe. Rais Magufuli pia amemshukuru Dkt. Adesina kwa kukubali AfDB kufadhili ujenzi wa miundombinu ya Jiji la Dodoma na kutoa Dola za Marekani Milioni 200 kwa ajili ya ujenzi wa uwanja mkubwa wa ndege wa kimataifa katika eneo la Msalato nje kidogo ya Jiji la Dodoma.

Mhe. Rais Magufuli amewaagiza wataalamu wa Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuharakisha mchakato wa kupata fedha hizo ili ujenzi wa uwanja uanze mara moja.

Mhe. Rais Magufuli amewashukuru Watanzania wote kwa kulipa kodi na kuiwezesha Serikali kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ikiwemo barabara ya Dodoma-Babati, na ametoa wito kwa wananchi kuitunza na vyombo vya ulinzi na usalama kuhakikisha vinachukua hatua dhidi ya waharibifu wa barabara na wanaosababisha ajali kwa kuvunja sheria za usalama barabarani.

Katika hatua nyingine Mhe. Rais Magufuli ameviagiza vyombo vya dola kuwatafuta wote waliohusika na upotevu wa shilingi Bilioni 2 kati ya Bilioni 2.8 zilizotolewa na Serikali tangu miaka ya 80 kutekeleza mradi wa maji wa Ntomoko kwa ajili ya wananchi wa kondoa lakini mpaka leo mradi huo haujatekelezwa.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewataka viongozi wa wilaya ya Kondoa kuacha migogoro baina yao na badala yake washughulikie Maendeleo na kero za Wananchi na amesisitiza kuwa “Nyie viongozi nimewateua mimi, acheni migogoro mkiendelea nitawatoa”.

Akiwa njiani kurejea Ikulu ya Chamwino Mhe. Rais Magufuli amekutana na wananchi wa Veyula katika Jiji la Dodoma na kuchangia shilingi Milioni 10 zitakazoungana na shilingi Milioni 5 zitakazotolewa na Mbunge wa Dodoma Mjini Mhe. Antony Mavunde na shilingi Milioni 1 zitakazotolewa na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma kwa ajili ya kujenga vyumba vya madarasa vya shule ya msingi Veyula.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2020 January 15, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 SHULE ZA BWENI (WASICHANA NA WANAUME) . December 20, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KATIBU TAWALA SINGIDA AKABIDHI OFISI KWA KATIBU TAWALA DODOMA

    March 23, 2023
  • MACHINGA DODOMA WAMPONGEZA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

    March 23, 2023
  • KIWANDA CHA AINA YAKE KUJENGWA KONGWA

    March 17, 2023
  • WAFANYAKAZI WAASWA MSHIKAMANO MAHALA PA KAZI

    March 15, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Mkoa akiongoza siku ya maombi jijini Dodoma
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.