• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

SOKO LA MACHINGA KUANZA RASMI OKTOBA 30

Imetumwa : October 26th, 2022

 


Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule, amefanya kikao na machinga wanaotarajiwa kufanya biashara katika soko la machinga lililopo barabara ya Bahi, lengo kuu likiwa kusikiliza na kutatua  kerozao.

Katika kikao hicho, Mkuu wa Mkoa ameongozana na Katibu Tawala Mkoa Dkt. Fatuma Mganga, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Mhe. Jabir Shekimweri, Kamati ya Ulinzi na usalama ya Wilaya pamoja na viongozi wanaosimamia soko hilo kutoka katika Halmashauri ya Dodoma Jiji.

Mkuu wa Mkoa, ameanza kikao kwa kusikiliza kero kadhaa zinazowakabili wakati wakisubiri kuhamia katika soko hilo. Miongoni mwa kero hizo ni pamoja na baadhi ya wafanya biashara kupangiwa vizimba ambavyo haviendani na biashara zao, baadhi ya machinga kukosa mikopo, machinga wa vitabu na magazeti kukosa vizimba, baba na mama lishe kukosa vizimba, daladala zianze kushusa abiria eneo hilo, n.k

Kero hizo zimepata majawabu kutoka kwa kaimu Mkurugenzi wa Jiji Bw. Msangi,  Mwenyekiti wa kamati ya kuratibu uhakiki wa Machinga  Bw. Joseph Bulali, ambaye alijibu hoja zilizojikita kwenye changamoto ya mama na baba lishe, vitambulisho vya machinga,maeneo ya wazi baada ya soko kufungwa,na ushuru.

Akijibu changamoto ya baadhi ya machinga kukosa mikopo, Katibu wa Soko la Machinga Bi. Sigirinda Mtemu, amesema kuwa, halmashauri zote zimekuwa zikitoa mikopo ya 10% kutoka mapato ya ndani mikopo ambayo mgawanyo wake ni 4% vijana, 4% wanawake na 2% watu wenye ulemavu.Sifa/ kigezo cha kuwawezesha vijana  kupata mkopo ni pamoja na umri ambao ni miaka 18-35, vijana hao wantakiwa wawe kwenye vikundi vya watu watano watano.Mpaka sasa tumevitambua vikundi 103 kila kikundi kikiwa na watu watano watano pamoja na watu wenye ulemavu 7.Changamoto ambao tunakutana nazo katika utoaji wa mikopo ni kuwa baadhi ya watu wameunda vikundi vya watu 5 ambapo ndani ya kundi hilo hakuna machinga hivyo kuwia vigumu kuwapatia mikopo hiyo.

Moja ya changamoto ambayo imeelezwa na machinga hao ni kuhusu ateja wao ambao wengi wataoka vyuo vya UDOM, MIPANGO, ST. JOHN, na eneo la Nzuguni na hivyo kumuomba mkuu wa mkoa kuwa mabasi ya kutoka maeneo hayo yawe yanafika kwenye kituo hicho kipya. Akijibu hoja hiyo Mkuu wa Mkoa amewataka LATRA kuhakikisha kuwa  kufikia tarehe Mosi Novemba, daladala zinapita njia ya  soko hilo na kunakua na kituo cha kupakia na kushusha abiria.

Mbali na majawabu ya kero, Mhe. Senyamule ametoa maagizo ya Serikali kwa kuwataka machinga hao kuwa tayari kuhamia kwenye soko hilo.

“Machinga tuwe tayari kuhamia hapa, tunakwenda kufanya biashara. Natoa wito kwenu tulitunze jengo hili kwani limegharimu fedha nyingi. Tufanye biashara kwa uaminifu na uadilifu, pasiwepo kuibiana na tutunze usafi wa mazingira” Amesisitiza  Mhe.Senyamule.

Aidha, amewataka Halmashauri ya Jiji kutatua kero zote zilizojitokeza na ambazo zitajitokeza hapo baadae “Jiji endeleeni kutatua kero hizi na zitakazojitokeza kwani maeneo bado yapo mengi endapo kama kutajitokeza upungufu wa vizimba watapangiwa maeneo mengine. Tunatamani kuiona Dodoma ambayo ni Fahari ya Watanzania  na soko hili tayari ni Fahari”

Vilevile, Mkuu wa Mkoa ametangaza rasmi tarehe ya machinga kuanza kuhamia kwenye soko hilo, ambayo ni kuanzia tarehe 28, 29 na 30 Oktoba, 2022 huku akiwataka viongozi wa Halmashauri ya Jiji kukaa eneo hilo siku zote hizo kwa ajili ya usimamizi wa zoezi hilo.

Naye Katibu Tawala Mkoa Dkt. Fatuma Mganga, amesema kuwa Dodoma tumebahatika kupata soko zuri na kuwataka machinga wasisite kuhamia sokoni hapo kwani milango ya kutatua changamoto haijafungwa. Pia amezungumzia suala la mikopo kwa wafanya biashara wadogo wadogo.

“Kuna mifuko zaidi ya 69 inayotoa mikopo kwa wafanyabiashara wadogo wadogo, pia kuna mabenki. Mutakapohamia hapa na kufahamika kwamba mnapatikana hapa kwa pamoja, mifuko hii pamoja na benki hizi zitawafuata hapa kuwahudumia. Naamini tunakwenda kuhamia kwa utulivu na Jiji letu linakwenda kuwa safi” Dkt. Mganga

MWISHO

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA MTIHANI WA MAARIFA (QT) 2020 January 15, 2021
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 SHULE ZA BWENI (WASICHANA NA WANAUME) . December 20, 2020
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA YA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • KATIBU TAWALA SINGIDA AKABIDHI OFISI KWA KATIBU TAWALA DODOMA

    March 23, 2023
  • MACHINGA DODOMA WAMPONGEZA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN

    March 23, 2023
  • KIWANDA CHA AINA YAKE KUJENGWA KONGWA

    March 17, 2023
  • WAFANYAKAZI WAASWA MSHIKAMANO MAHALA PA KAZI

    March 15, 2023
  • Tazama Zote

Video

Mkuu wa Mkoa akiongoza siku ya maombi jijini Dodoma
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.