• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

TAWLA - SAUTI YA WANAWAKE NA WATOTO WALIOKOSA ULINZI WA KISHERIA KATIKA JAMII

Imetumwa : May 3rd, 2025

Na. Hellen M. Minja,

       Habari - DODOMA RS

Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania, TAWLA, kimetajwa kuwa sauti ya Wanawake na watoto waliokosa ulinzi wa kisheria,ikiwa ni pamoja na kuchochea mabadiliko ya kisheria,kuondoa Sheria kandamizi zilizokua zinawakabili Wanawake na watoto ndani ya Jamii.

Hayo yamesemwa leo Mei 03, 2025 na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule wakati wa hafla fupi ya kusherehekea miaka 35 tangu kuanzishwa kwa Chama hicho iliyokwenda sambamba na uzinduzi wa jengo la ofisi yao Mkoani hapa lililopo eneo la Ilazo Jijini Dodoma.

"Natoa pongezi kwa kazi kubwa iliyofanywa na TAWLA ambapo mmekua sauti ya Wanawake na watoto waliokosa Ulinzi wa kisheria lakini pia mmechochea mabadiliko ya kisheria kwenye Sheria kandamizi, mmefanya tafiti zenye mchango mkubwa katika Sera, mmesaidia Wanawake, watoto na jamii kwa ujumla kupata elimu ya kisheria"  

Kadhalika, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TAWLA Bi. Suzan Ndomba, amesema maendeleo ya Taifa hayawezi kufikiwa pasi na usawa wa kijinsia kwani Wanawake ni kiungo muhimu katika maendeleo, na nchi haiwezi kuendelea kama wasiposhirikishwa katika nyanja za Siasa, Uchumi, Elimu na Sheria.

Vile vile, Msajili wa Mabaraza ya Ardhi na Nyumba Wilaya Bi. Stella Tullo, ameongeza kuwa  miongoni mwa kesi wanazozipokea kwenye Mabaraza hayo ni za Wanawake hivyo, wanapopata Wanawake ambao hawana uwezo wa kulipia huduma za Wanasheria, TAWLA imekua msaada mkubwa kwa Wanawake hao wakati wote.

Akizungumzia namna walivyopata ofisi hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TAWLA Bi. Tike Mwambipile, amesema awali walikua na eneo lililopitiwa na Mradi wa SGR hivyo walilipwa fidia ya Milioni 42 iliyowezesha kupata eneo jipya la sasa ambapo walijenga ofisi na kuhamia rasmi 2024 na waliona ni vyema kulizindua rasmi katika sherehe ya miaka 35 ya Chama hicho.

Maadhimisho ya miaka 35 ya TAWLA yamekwenda sambamba na kauli mbiu za "Miaka 35 ya Haki na usawa"  pamoja na "Haki haina jinsia" zote zikihamasisha na kutoa ujumbe kwamba utoaji haki hauchagui jinsia, kila mmoja ana haki sawa ya kupata msaada wa kisheria pindi anapouhitaji.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • DODOMA YADHAMIRIA KUJIKITA KWENYE KILIMO CHA MATUFAHA (APPLES) KUINUA UCHUMI

    May 08, 2025
  • MAAFISA MAZINGIRA WAPEWA HEKO NA RAS MMUYA

    May 06, 2025
  • RAS MMUYA AFUNGUA KIKAO KAZI CHA MAAFISA UTUMISHI MKOA WA DODOMA

    May 05, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.