• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

WAMILIKI WA MAABARA BINAFSI WATAKIWA KUTOA MAJIBU SAHIHI YA VIPIMO KWA WAGONJWA

Imetumwa : June 17th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Wamiliki wa Maabara binafsi Mkoa wa Dodoma, wametakiwa kutowalazimisha Wataalam wa Maabara kutoa majibu yasiyo sahihi ya vipimo vya magonjwa kwa dhana ya kuuza aina fulani ya dawa kutokana na kushinikiza kupima magonjwa kinyume na utaratibu.

Hayo yamesemwa na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma Bw. Kaspar K. Mmuya alipokua akifunga Mkutano kati ya ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Wamiliki wa Maabara binafsi za afya na Wataalamu wa Maabara uliofanyika Juni 16, 2025 kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Jijini humu.

Akizungumza wakati wa kufunga Mkutano huo uliolenga kufanya tathmini ya utoaji huduma za Maabara ikiwemo uwasilishwaji wa changamoto wanazokutana nazo wataalam hao kwenye vituo vyao vya kazi, Bw. Mmuya alisema;

“Tusing’ang’anize wagonjwa kupima vitu ambavyo havipo kwenye utaratibu, Jingine, kutoa majibu ambayo yanapelekea dawa fulani iuzike, sisi tukiandikiwa dawa lazima tumeze kwa sababu tunataka tupone. Hii sio sawa, tusitoe majibu yasiyo sahihi ndio hoja yangu”.

Akifungua Mkutano huo, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Thomas Rutachunzibwa, amesema kuwa kwa takribani miaka miwili Mkoa wa Dodoma umeshuhudia maboresho makubwa katika sekta ya afya ambapo Serikali imewekeza takribani shilingi Bilioni 80.25 kwa upande wa miundombinu, vifaa tiba na dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya.

Kadhalika, Msajili kutoka Bodi ya Maabara binafsi za Afya (PHLB) Bw. Dominic Fwiling’afu amewakumbusha Wataalam hao kuwa Sera na kauli mbiu ya Serikali kwa sasa ni ubora wa huduma kwani Serikali imefanya mengi lakini ubora wa huduma ni jukumu lao na wataalamu hao ambao ni Wadau muhimu wa sekta ya Afya.

Aidha, Msimamizi wa Huduma za Maabara Mkoa wa Dodoma Bw. Garadina Challe amesema wamiliki wa Maabara binafsi wanatakiwa kufahamu kuwa Maabara za Afya ni uti wa mgongo katika kutoa matibabu kwa wagonjwa,hivyo amewataka wazingatie mikataba na wataalam wao kulingana na miongozo sambamba na kulipa tozo za Serikali kwa wakati.

Hata hivyo, Afisa Ubora kutoka Bodi ya Maabara Binafsi za Afya Bw. Berzard Ngumbuchi, amesema katika kuboresha huduma za Maabara Binafsi za Afya, Sheria, Kanuni na Miongozo imezingatia utaratibu wa kusajili, kuratibu na kukagua ili kuhakikisha viwango vinatumika, kuzingatiwa na kuimarika wakati wote.

Mkutano huo wa siku moja, umeazimia mambo kadhaa ikiwemo upatikanaji wa mifuko ya damu (blood bag) katika vituo vya kutolea huduma za afya, upatikanaji wa vitendanishi vya kupimia ugonjwa wa Kifua Kikuu kwa njia ya Hadubini, kuhuisha taarifa za vituo kwenye Mfumo wa usajili wa kutolea huduma za afya na kuwasilisha orodha ya vituo vyote vya kutolea huduma za afya vilivyofungwa kwa Mratibu wa Mkoa.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • RAS MMUYA AWAAHIDI ZAWADI NONO WANAMICHEZO - UMITASHUMTA

    June 17, 2025
  • WAMILIKI WA MAABARA BINAFSI WATAKIWA KUTOA MAJIBU SAHIHI YA VIPIMO KWA WAGONJWA

    June 17, 2025
  • TAASISI ZA UMMA ZATAKIWA KUJIUNGA NA MFUMO KURAHISISHA HUDUMA KWA WANANCHI

    June 17, 2025
  • DODOMA MOTO MKALI MASHINDANO UMITASHUMTA

    June 14, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.