• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

BARABARA YA IRINGA JIJINI DODOMA MBIONI KUPANULIWA KUDHIBITI MSONGAMANO

Imetumwa : September 17th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Serikali ipo mbioni kufanya upanuzi wa Barabara ya Iringa inayopita kwenye Kituo cha Reli ya Kisasa ya mwendokasi (SGR) Mkoa wa Dodoma, Dkt. Samia Suluhu Hassan katika eneo la Mkonze Jijini hapa kwa lengo la kudhibiti kero ya msongamano wa magari, Bajaji na Pikipiki hali inayosababisha kadhia kwa watumiaji wa Barabara hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule amebainisha hayo wakati akijibu kero iliyoibuliwa wakati wa Semina maalum iliyoandaliwa na Ofisi yake kwa lengo la kutoa elimu, kusikiliza na kutatua kero za Maafisa Usafirishaji wa Bajaji na Pikipiki (Bodaboda) wa Jiji la Dodoma iliyofanyika Septemba 17, 2025 katika Ukumbi wa Jengo la Safina.

Kero hiyo iliyoibuliwa na moja ya Maafisa hao akilalamikia msongamano mkubwa wa vyombo vya usafiri katika eneo hilo hali inayosababisha ajali mara kadhaa kutokana na uwepo wa Kituo hicho cha Reli ambacho kinapokea watu wanaoingia na kutoka kwa wingi Jijini hapa kutoka Mikoa ya Dar es Salaam na Morogoro.

“Barabara ya SGR inakwenda kutanuliwa na kuwa na njia nne badala ya mbili ambazo zipo sasa hivi ili kuepusha ajali zinazojitokeza mara chache katika eneo hilo pia kuondoa msongamano wa magari na vyombo vingine vya moto kutokana na uwepo wa Kituo cha reli hapo”. Amesema Mhe. Senyamule.

Aidha, Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mhe. Jabir Shekimweri alipokua akijibu kero ya vitendo vya ukiukwaji wa sheria barabarani wanavyodai kufanyiwa Maafisa hao, amesema Jiji lipo kwenye zoezi endelevu la ufungaji wa CCTV Kamera kwa usalama na zitasaidia kuondoa uovu unaodaiwa kwani matukio yote yataonekana kutokana na Mfumo huo kuwa wa wazi kwa wote.

Akiwasilisha mada juu ya mchango wa Maafisa usafirishaji (Bodaboda) kwenye usalama wa Mkoa, Mkuu wa usalama barabarani Mkoa wa Dodoma (RTO) Yusuph Kamote amesema Maafisa hao wamekua walinzi shirikishi madhubuti kwani wamekua wakitoa taarifa za uhalifu pindi zinapotokea na kusaidia Mamlaka husika kufika eneo husika kwa wakati.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva Bajaji na Pikipiki Jiji la Dodoma (UMAPIDO) Bw. Chacha Marwa  ameishukuru  Serikali  kwa  kuendelea kuwapatia mafunzo,kuwashirikisha katika masuala mbalimbali pamoja na kutatua changamoto zao.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

Matangazo

  • No records found
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • BAHI WAPEWA HEKO UJENZI MIRADI YA ELIMU

    October 08, 2025
  • “TUSIMAME IMARA JUU YA KULINDA AMANI YA NCHI YETU - RC SENYAMULE

    October 07, 2025
  • DKT. KAZUNGU ATOA WITO KWA WADAU WA TAKWIMU KUZINGATIA USAHIHI

    October 07, 2025
  • JIJI LA DODOMA KUNUFAIKA NA TEKNOLOJIA KUTOKA JAMHURI YA CZECH

    October 07, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.