• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

BILLIONI 14 KUJENGA OFISI ZA UBALOZI WA UGANDA JIJINI DODOMA

Imetumwa : May 9th, 2025

Na. Sizah Kangalawe- Dodoma RS

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule Mei 09/ 2025 ameshiriki hafla ya uwekaji  jiwe la msingi ujenzi wa ofisi za ubalozi wa Uganda Nchini, zinazojengwa katika mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma.

Akizungumza na washiriki wa hafla hiyo Senyamule ameweka bayana kuwa ujenzi wa ofisi za Mabalozi  Jijini Dodoma unatokana na uwepo wa miundombinu rafiki inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya Sita Chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

‘’Ni baraka kubwa kwetu kama Mkoa, kuona watu wameielewa Serikali  kuwa Dodoma ndio makao makuu, na wameamini hata wao wa ngazi za Ubalozi na diplomasia wanaweza kuishi Dodoma,hilo ni jambo la faraja kwetu.

"Hii yote inatokana na uwekezaji wa Serikali uliofanywa na Rais wetu ambaye amewekeza fedha nyingi, sio tu kwenye mji wa Serikali lakini huduma mbalimbali zinazowarahisishia kufika Dodoma, huduma  nzuri za afya pamoja na ujenzi wa Uwanja wa ndege wa kimataifa Msalato ambao utawawezesha mabalozi kutua Dodoma moja kwa moja kutoka nchi mbalimbali", amesema Senyamule

Kwa upande wake Balozi wa Uganda nchini Tanzania Mhe. Kanali Fred Mwesigye ameeleza kuwa ujenzi huo si tu  jengo la kuhudumia wananchi bali ni kituo muhimu cha kuimarisha na kukuza zaidi uhusiano wa kiuchumi na kidiplomasia baina ya Tanzania na Uganda.

 Aidha Balozi mwesigye amesema Uganda inaona fahari kutumia fursa hiyo kuwa nchi ya kwanza kuanzisha ujenzi wa Ofisi ya Ubalozi ikiwa ni sehemu ya kutoa shukrani zake kwa Serikali ya Tanzania kwa mchango iliyoutoa katika ujenzi wa Taifa la Uganda.

Hata hivyo RC Senyamule  ametumia fursa hiyo kuzihimiza Balozi zingine zilipo Nchini, kuhamishia ofisi zao Jijini Dodoma, kwa kuwa Serikali tayari imeshaweka mazingira rafiki na wezeshi ya kuwawezesha kutekeleza majukumu yao vyema wakiwa Jijini hapa.

ujenzi wa Ofisi za Ubalozi huo utagharimu zaidi ya billioni 14 za Kitanzania na unatarajiwa kukamilika ndani ya miaka miwili.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • BILLIONI 14 KUJENGA OFISI ZA UBALOZI WA UGANDA JIJINI DODOMA

    May 09, 2025
  • WAZAZI WASISITIZWA KUPELEKA WATOTO SHULE KUFUATIA KUIMARIKA KWA MIUNDOMBINU YA ELIMU

    May 08, 2025
  • WATUMISHI HODARI 2025 KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA WAPONGEZWA

    May 09, 2025
  • MRADI WA KUIMARISHA HUDUMA ZA KIFAFA WAZINDULIWA DODOMA

    May 08, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.