• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

BILLIONI 3 KUTUMIKA KUJENGA CHUMBA CHA UANGALIZI WA WATOTO WACHANGA JIJINI DODOMA

Imetumwa : June 10th, 2025

Na. Hellen M. Minja

       Habari – DODOMA RS

Katika jitihada za kutokomeza vifo vya watoto wachanga wakati wa kuzaliwa, Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, inatarajia kujenga chumba cha uangalizi maalumu kwa watoto wachanga wanaozaliwa na changamoto za kiafya ‘Neo-natal Intesive Care Unit (NICU)’ kwa thamani ya shilingi bilioni tatu katika Mkoa wa Dodoma.

Hayo yamebainishwa na Waziri mwenye dhamana ya Afya Mhe. Jenista Mhagama wakati wa hafla ya kupokea taulo za watoto wachanga zilizotolewa na Kampuni ya Sunda International inayotengeneza taulo za kike za ‘Soft care’ zitakazogawiwa kwenye Hospitali za Wilaya za Mkoa wa Dodoma. Hafla hiyo imefanyika kwenye viwanja vya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma Juni 09, 2025.

“Mhe. Rais ameagiza niwaletee bilioni tatu kujenga ICU mpya kwa ajili ya watoto wachanga tu, hiyo kazi yake itakua ni moja tu, kuhakikisha wale watoto waliozaliwa kwa dharura na hasa wenye magonjwa, changamoto za utoto ikiwa ni pamoja na uzito ambao ni pungufu, wanatengenezewa mahali maalumu ambapo watapata uangalizi wa karibu na kuokoa maisha yao”.

Ameongeza kuwa katika kupanua na kuboresha huduma kwenye vituo vya afya, Serikali pia inatoa kiasi cha shilingi Bilioni 7 kukarabati upya Kituo cha Afya Makole cha Jijini Dodoma ambapo ukarabati huo utajikita kwenye eneo la uzazi ili kuwa na mahali salama kwa ajili ya kina Mama kujifungulia.

Akitoa salamu za Mkoa kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule ameelezea namna Serikali ilivyotoa fedha kwenye sekta ya afya ndani ya Mkoa wake.

“Dodoma tulipata zaidi ya bilioni 80.25 katika sekta ya afya ambapo katika hizo, shilingi bilioni 42.13 zilitumika kwa ajili ya miundombinu ya vituo vya afya, bilioni 38.1 zilitumika kwa ajili ya ununuzi wa dawa, vifaa tiba, mashine na vitenganishi. Sasa hivi upatikanaji wa dawa katika Mkoa wetu ni wa kiwango kikubwa kwani katika Halmashauri ni kati ya 85% mpaka 98% watu wakienda vituoni”.

Mhe. Senyamule pia, ametoa msisitizo kwa Waganga  Wakuu wa Wilaya waliopo kwenye Halmashauri zitazokabidhiwa vifaa hivyo, kuhakikisha wanavifikisha kwa kadri ilivyokusudiwa kwa watu wenye changamoto ya kupata taulo hizo na utafanyika ufuatiliaji kuona kama jambo hilo limefanyika kama lilivyokusudiwa kutokana na ukubwa wa changamoto hiyo.

Aidha, Mkurugenzi Mtendaji wa ‘Sunda International’ kwa upande wa Tanzania Bw. Andy Lui, amesema kampuni yake imetoa taulo za watoto wachanga na kina mama waliotoka kujifungua zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 65 ambapo tukio hilo limeinua uzalishaji wa bidhaa pamoja na uchumi wa ndani.


#dodomafahariyawatanzania

#wekezadodomastawishadodoma

#keroyakowajibuwangu

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA JIJI LA DODOMA YAPONGEZWA KUPATA HATI SAFI KWA MWAKA 2023/2024

    June 13, 2025
  • KIWANDA CHA NONDO KINACHOTUMIA UMEME JUA KUJENGWA CHAMWINO MKOANI DODOMA

    June 13, 2025
  • RAIS DKT. SAMIA KUFANYA ZIARA JIJINI DODOMA

    June 13, 2025
  • DODOMA YAENDELEA NA MAANDALIZI KUELEKEA SIKU YA KUPINGA DAWA YA KULEVYA DUNIANI

    June 12, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.