• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Ofisi |
    • Malalamiko |
    • eoffice |
Dodoma Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Muundo wa Taasisi
      • Huduma Zetu
    • Huduma Zetu
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Seksheni
      • Administration and Human Resource Management Section
      • Planning and Coordination
      • Infrastructure section
      • Management Monitoring and Inspection section;
      • Education and vocational Training section
      • Economic and productive sectors section;
      • Health, Social welfare and Nutrition services section
      • Industry, Trade and Investment section
    • Vitengo
      • Information Communication Technology (lcT) and Statistics
      • Government Communication Unit
      • Finance and Accounts unit;
      • Internal Audit unit
      • Legal services unit;
      • Procurement Management unit;
  • Wilaya
    • Bahi
    • Chamwino
    • Kongwa
    • Mpwapwa
    • Kondoa
    • Dodoma Mjini
    • Chemba
  • Mamlaka za Serikali za mitaa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Bahi
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
    • Halmashauri ya Wilaya ya Chemba
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa
    • Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa
    • Halmashauri ya Wilaya Mpwapwa
    • Halmashauri ya Mji Kondoa
    • The City Council of Dodoma (CCD)
  • Uwekezaji
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu Mbalimbali
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Habari kwa Umma
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

HALMASHAURI ZA MKOA WA DODOMA ZAPOKEA VIFAA VYA USAMBAZAJI CHANJO

Imetumwa : January 10th, 2025

Na. Hellen M. Minja,

      Habari – DODOMA RS

Katika juhudi za kuendelea kuimarisha sekta ya huduma za afya Nchini, Serikali ya Tanzania imetoa gari moja na pikipiki 13 kwa sekta hiyo Mkoa wa Dodoma zitakazotumika katika usambazaji wa chanjo ambazo zimekabidhiwa leo Januari 10, 2025 kwa Wakuu wa Wilaya za Mkoa huu.

Hafla ya kukabidhi gari na pikipiki hizo imefanywa na   Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Rosemary Senyamule katika viwanja vya ofisi yake jengo la Mkapa Jijini Dodoma ambapo amesisitiza kuwa dhamira ya Rais ni Watanzania wapate huduma bora.


“Mhe. Rais anayo dhamira ya kuona Watanzania wanapata huduma bora za afya. Vifaa hivi tuendelee kuvitumia kwa utashi mkubwa kuhakikisha Wanadodoma wanafurahia huduma tunazowapa sisi watumishi wa sekta ya afya kwani gari hili na pikipiki zitasaidia kufikisha vifaa haraka” Mhe. Senyamule.


Awali, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dr. Thomas Rutachunzibwa, aliainisha mgawanyo wa vifaa hivyo kwa Halmashauri zote 8 za Mkoa wa Dodoma ambapo Bahi imepata pikipiki 1, Chamwino 2 kwenye Kituo cha Itiso, Chemba pikipiki 2 kwenye Zahanati ya Laboda, Dodoma Jiji imepata gari moja, Kondoa DC pikipiki 2 kwenye Zahanati ya Chololo, Kondoa Mji pikipiki 1, Kongwa pikipiki 2 kwenye Kituo cha Afya Chitego na Mpwapwa imepata pikipiki 2 kwenye kituo cha Chipogolo.


Nae, Mratibu wa huduma za chanjo Mkoa wa Dodoma Bw. Francis Bujiku, amesema kuwa gari na pikipiki hizo vitakwenda kuboresha huduma za chanjo kwa Mkoa wa Dodoma na kurahisisha ufuatiliaji wa magonjwa yanayozuilika kwa chanjo ambapo awali ilikua vigumu kuwafikia wananchi wanaoishi maeneo ya pembezoni.


Mwezi Desemba, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, ilipokea taarifa kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI kuhusu mgao wa Gari moja na pikipiki 13 kwa Halmashauri kwa ajili ya usimamizi wa huduma za chanjo ambapo vifaa hivyo vilinunuliwa na Wizara ya Afya chini ya ufadhili wa shirika la GAVI.




#dodomafahariyawatanzania                                                    

#keroyakowajibuwangu                                                                          

#mtiwangubirthdayyangu

Matangazo

  • "WANANCHI JITOKEZENI MAPOKEZI YA MWENGE WA UHURU 2025" - RC SENYAMULE February 17, 2025
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • WATUMISHI HODARI 2025 KUTOKA OFISI YA MKUU WA MKOA WA DODOMA WAPONGEZWA

    May 09, 2025
  • MRADI WA KUIMARISHA HUDUMA ZA KIFAFA WAZINDULIWA DODOMA

    May 08, 2025
  • UBALOZI WA UINGEREZA NCHINI TANZANIA WAADHIMISHA MAFANIKIO YA MWAKA MMOJA NCHINI

    May 08, 2025
  • MAANDALIZI YA ‘ DIPLOMATIC CAPITAL CITY TOUR’ YAIVA

    May 08, 2025
  • Tazama Zote

Video

RC SENYAMULE AKIZUNGUMZA KWENYE UZINDUZI WA SERA YA ELIMU NA MAFUNZO YA MWAKA 2014 TOLEO LA 2023.
Video Nyinginezo

Kurasa za Karibu

  • Speeches
  • mission and vision
  • Photo Gallery
  • Videos
  • Press Releases
  • Organization Structure
  • Reports
  • Client Service Charter
  • Acts

Tovuti Muhimu

  • PO-RALG
  • Public Service Management
  • Parliament of Tanzania
  • UDOM
  • Government Portal
  • Prime Minister's Office Website

World Visitors Tracker

world map hits counter

Rejesta ya Watembeleaji

free HitCounter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Jengo la Mkapa (Mkapa House) Barabara ya Hospitali ya Mkoa

    Anuani ya Posta: 914 DODOMA

    Simu: +255 26 232 4343/232

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ras@dodoma.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya eneo

Hakimiliki©2016 GWF . Haki zote zimehifadhiwa.